• HABARI MPYA

  Jumapili, Julai 22, 2018

  SIMBA SC WAPO ANGANI WANAITAFUTA UTURUKI, MBELGIJI ANA WIKI MBILI ZA KUISUKA TIMU YA USHINDI

  Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
  KIKOSI cha Simba SC kimeondoka Aflajiri ya leo kwenda Uturuki kuweka kambi ya muda wa wiki mbili kujiandaa na Ligi Kuu ya Tanzania bara inayotarajiwa kuanza Agosti 22, mwaka huu.
  Simba SC imeondoka na wachezaji wote iliyowasajili kwa ajili ya msimu ujao chini ya kocha wake mpya, Mbelgiji Patrick J. Aussems atakayekuwa chini ya Msaidizi Mrundi, Masoud Juma aliyekuwa Msaidizi pia wa makocha wawili waliopita, Mcameroon Joseph Omog na Mfaransa, Pierre Lechantre.
  Ikiwa nchini Uturuki, Simba SC itapata mazoezi katika mazungira na viwanja bora, pamoja na mechi za kirafiki za kujipima nguvu kabla ya kurejea nchini kwa ajili ya tamasha la Simba Day Agosti 8 Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
  Wachezaji wa Simba SC kutoka kulia Nicholas Gyan, Jonas Mkude na James Kotei wakiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kabla ya safari yao na chini wakiwa kwenye ndege Wachana watupu Kotei, Gyan na Asante Kwasi 
  Ikumbukwe Simba SC, mabingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania watauanza msimu kwa mchezo wa wa Ngao ya Jamii dhidi ya washindi wa Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu Azam Sports Federation Cup (ASFC), Mtibwa Sugar Agosti 18, mwaka huu Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.               
  Katika Ligi Kuu, Simba itaanza na Tanzania Prisons Agosti 22, mechi itakayochezwa Saa 1:00 usiku Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
  Na watakutana na mahasimu wao wa jadi, Yanga watakutana Septemba 30, mwaka huu katika mechi ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kuanzia Saa 10:00 jioni Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA SC WAPO ANGANI WANAITAFUTA UTURUKI, MBELGIJI ANA WIKI MBILI ZA KUISUKA TIMU YA USHINDI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top