• HABARI MPYA

  Jumatatu, Julai 23, 2018

  YAHYA ZAYED WA AZAM FC AENDA KUFANYA MAJARIBIO BIDVEST WITS AFRIKA KUSINI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI wa Azam FC, Yahya Zayed ameondoka leo mjini Dar es Salaam kwenda Afrika Kusini kufanya majaribio ya kujiunga na klabu ya Bidvest Wits ya huko.
  Zayed ameondoka nchini siku mbili tu baada ya kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia Azam FC – maana yake Bidvest ikiridhishwa naye italazimika kumnunua.
  Zayed ameondoka nchini kiasi cha wiki mbili tangu aisaidie Azam FC kutwaa taji la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe la Kagame.

  Yahya Zayed (katikati) ameondoka leo mjini Dar es Salaam kwenda Afrika Kusini kufanya majaribio Bidvest Wits 

  Azam FC iliichapa Simba SC mabao 2-1 na kubeba Kombe la Kagame Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam wiki iliyopita, hiyo ikiwa ni mara ya pili kwao kutwaa taji hilo baada ya mwaka 2015.
  Na Zayed anakuwa mchezaji wa pili kutoka kikosi cha Azam FC kilichotwaa Kombe la Kagame baada ya mshambuliaji mwingine, Shaaban Iddi Chilunda ambaye amechukuliwa kwa mkopo na Tenerife ya Daraja la Kwanza Hispania.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YAHYA ZAYED WA AZAM FC AENDA KUFANYA MAJARIBIO BIDVEST WITS AFRIKA KUSINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top