• HABARI MPYA

  Jumatano, Julai 25, 2018

  SINGIDA UNITED YASAJILI WACHEZAJI WATATU WAPYA AKIWEMO JAMAL MWAMBELEKO WA SIMBA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Singida United imesajili wachezaji watatu wapya Jumanne kutoka timu mbalimbali wapinzani wa Ligi Kuu ili kukiongezea kikosi chake msimu ujao. 
  Hao ni beki wa kushoto anayeweza kucheza kama kiungopia, Jamal Mwambeleko kutoka Simba SC ya Dar es Salaam aliyesaini mkataba wa mwa mmoja, beki wa kati Rajab Zahir kutoka Ruvu Shooting ya Pwani aliyesaini mkataba wa miaka miwili na mshambuliaji chipukizi, Athanasi Mdamu aliyesaini mkataba wa miaka mitatu kama mchezaji huru.
  Mkurugenzi wa Singida United, Sanga Festo amesema kwamba Athanas amejiunga kama na klabu hiyo kama mchezaji huru baada ya kumaliza masomo yake katika shule ya Alliance mjini Mwanza na Mwambeleko ametua Namfua baada ya mazungumzo mazuri na klabu yake, Simba SC.
  Mkurugenzi wa Singida United, Sanga Festo (kulia) akimkabidhi jezi ya timu hiyo Jamal Mwambeleko (kushoto) 
  Mkurugenzi wa Singida United, Sanga Festo (kulia) akimkabidhi jezi ya timu hiyo Athanas Mdamu (kushoto)
  Mkurugenzi wa Singida United, Sanga Festo (kulia) akimkabidhi jezi ya timu hiyo Rajab Zahir (kushoto)

  “Ni matumaini yangu kabisa wachezaji hawa wapya watakiwa na msaada mkubwa kwa kikosi chetu msimu ujao katika kuwania mataji,”amesema Sanga.
  Singida United imeweka kambi mjini Mwanza kujiandaa na msimu ujao wa Ligi Kuu y Tanzania Bara, ikitoka kushiriki michuano ya SportPesa Super Cup na Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe la Kagame.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SINGIDA UNITED YASAJILI WACHEZAJI WATATU WAPYA AKIWEMO JAMAL MWAMBELEKO WA SIMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top