• HABARI MPYA

    Monday, July 23, 2018

    OZIL ASTAAFU UJERUMANI SABABU YA UBAGUZI NA KUFANYWA 'MBUZI WA KAFARA'

    KIUNGO Mesut Ozil amestaafu soka ya kimataifa akilalamikia kufanyiwa ubaguzi na Chama cha Soka Ujerumani baada ya kufanywa mbuzi wa kafara kufuatia timu ya taifa kutolewa mapema kwenye fainali za Kombe la Dunia. 
    Katika taarifa yake ndefu, mchezaji huyo wa Arsenal mwenye umri wa miaka 29, amesema kwamba amegeuzwa kuwa 'propaganda za kisiasa' na na hajivunii tena kuvaa jezi ya timu ya taifa.
    Ozil amejikuta akishambuliwa mno baada ya Ujerumani kutolewa raundi ya kwanza kwenye fainali za Kombe la Dunia nchini Urusi, matokeo yao mabaya zaidi kwenye fainali za Kombe la Dunia ndani ya miaka 80, yaliyotokea baada ya kupigwa picha akiwa na rais mtata wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan.

    Mesut Ozil amestaafu kuchezea Ujerumani baada ya kufanywa mbuzi wa kafara kufuatia timu ya taifa kutolewa mapema kwenye fainali za Kombe la Dunia 

    Ameposti barua tatu za wazi kwenye mitandao ya kijamii jana, ya mwisho ikithibitisha kudtaafu kwake soka ya kimataifa akilalamikia ubaguzi na kuvunjiwa heshima.
    Ozil, ambaye ni mchanganyiko wa Ujerumani na Uturuki, alisema jana kwamba yeye na familia yake wamepokea barua pepe za chuki, simu za vitisho na kukashifiwa kwenye mitandao ya kijamii..
    Katika taarifa yake aliyoposti Twitter: ameandika; "Mambo niliyofanyiwa na DFB (Shirikisho la Soka Ujerumani) na wengine wengi yamenifanya nisitake tena kuvaa jezi ya Ujerumani,".
    "Nahisi sitakiwi na ninafikiri kwamba nilichovuna tangu nilipoanza kucheza soka ya kimataifa mwaka 2009 kimesahaulika," amesema Ozil ambaye alikuwemo kwenye kikosi cha Ujerumani kilichotwaa Kombe la Dunia nchini Brazil mwaka 2014.
    "Sitachezea tena Ujerumani kwenye soka ya kimataifa baada ya ubaguzi huu na kuvunjiwa heshima. Nimekuwa nikivaa jezi ya Ujerumani kwa kujivunia na kuvutiwa, lakini sasa hapana,".
    "Kwa walichonifanyia viongozi wakubwa wa DFB, kuidharau asili yangu ya Uturuki na kuleta ubinafsi kwa kuniingiza mimi kwenye propaganda za kisisa, sasa inatosha ni inatosha,".
    "Hiki sicho kinachonifanya nicheze soka, na sitabaki nyuma na kufanya chochote juu ya hili. Ubaguzi hauwezi, daima kukubaliwa. Mimi ni Mjerumani tunaposhinda, lakini si raia tunapofungwa,".
    "Sitasimama tena kuwa mbuzi wa kafara wa watu wasiojiweza na kuweza kutekeleza majukumu yao kwa usahihi,". 
    "Kuna kigezo cha Mjerumani kamili ambacho sitimizi? Rafiki zangu Lukas Podolski na Miroslav Klose hawajawahi kuzungumziwa kama Wajerumani - Wapoland, hivyo kwa nini mimi ni Mjerumani - Mturuki? Ni kwa sababu mimi Mturuki? Ni kwa sababu mimi ni Muislamu?'
    Mapema Ozil alitoa utetezi wake juu ya kukutana na rais wa Uturuki, Erdogan, akisema kwamba kukataa kukutana naye ingekuwa kuwakosea adabu wazee wake.
    Ozil, ambaye wakati wote amekuwa akijivunia asili ya Uturuki alimkabidhi Erdogan jezi iliyosainiwa ya Arsenal walipokutana naye mjini London mwezi Mei, mwaka huu. Aliambatana na Ilkay Gundogan, ambaye pia ana asili ya Uturuki na mshambuliaji wa Everton, Cenk Tosun.
    Akiwa na nguvu zaidi nchini Uturuki, Rais Erdogan amekuwa akichukuliwa kama dikteta wa kisasa mbele ya wapinzani wake na ziara yake ya siku mjini London alikutana na makundi ya wa[ogania haki za binadamu.
    Kukutana ghafla kwa Ozil na Rais wa Uturuki kulimletea matatizo katika timu ya taifa na kocha Oliver Bierhoff akapendekeza aenguliwe kwenye kikosi cha Kombe la Dunia.
    Pamoja na hayo, Ozil akasema kwamba mkutano wake na Erdogan zaidi ulikuwa kuonyesha heshima na kulipa fadhila kwa nchi yake ya asili kuliko mtu huyo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: OZIL ASTAAFU UJERUMANI SABABU YA UBAGUZI NA KUFANYWA 'MBUZI WA KAFARA' Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top