• HABARI MPYA

  Jumatatu, Julai 23, 2018

  WACHEZAJI WATATU WENGINE WALIOIPANDISHA KMC LIGI KUU WAPEWA MIKATABA MIPYA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni (KMC) imeendelea kuwapa mikataba mipya wachezaji wake waliopandisha timu kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya leo kuwasainisha vijana wake watatu. 
  Meneja wa KMC, Walter Harrisons ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online kwamba wachezaji hao ni beki wa pembeni Ally Ramadhani, mshambuliaji Rehan Kibingu na kiungo mshabuliaji Cliff Buyoya wote wakipewa kandarasi ya mwaka mmoja.
  “Hawa ni baadhi ya wachezaji waliokuwa na timu daraja la kwanza na kuisadia kupanda ligi huu,”amesema Harisson.
  Cliff Buyoya (kulia) akifurahia na Meneja, Walter Harrison baada ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja 

  Watatu hao wanafanya idadi ya wachezaji waliopewa mikataba mipya kutoka kikosi kilichopandisha timu kutoka Daraja la Kwanza chini ya kocha Freddy Felix Minziro kufika sita, baada ya viungo Abdulhalim Humud na Adam Kingwande waliowahi kuchezea klabu ya Simba na Rayman Mgungila aliyewahi kuchezea Azam FC.

  KMC pia imesajili wachezaji wanne wapya ambao ni kipa Juma Kaseja kutoka Kagera Sugar na mabeki Aaron Lulambo, Ali Ali wote kutoka Stand United, Sadallah Lipangile kutoka Mbao FC na kiungo mshambuliaji, Abdul Hillary Hassan kutoka Tusker FC ya Kenya.
  Tayari Minziro amekwishaondolewa na nafasi yake imechukuliwa na Mrundi Ettienne Ndayiragijje ambaye misimu miwili iliyopita alikuwa Mbao FC ya Mwanza.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: WACHEZAJI WATATU WENGINE WALIOIPANDISHA KMC LIGI KUU WAPEWA MIKATABA MIPYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top