• HABARI MPYA

  Jumatatu, Julai 23, 2018

  KILIMANJARO QUEENS YAZINDUKA KOMBE LA CHALLENGE, YAICHAPA UGANDA 4-1

  Na Somoe Ng'itu, KIGALI
  MABINGWA watetezi wa mashindano ya soka ya Kombe la Challenge kwa wanawake timu ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Queens leo wameshinda mabao 4-1 dhidi ya Uganda katika mechi iliyofanyika kwenye Uwanja wa Kigali, Nyambirambo jijini hapa.
  Kutokana na ushindi huo, Kilimanjaro Queen imefikisha pointi nne huku Uganda waliokuwa kileleni kabla ya mechi ya jioni kati ya Rwanda na Ethiopia.
  Kilimanjaro Queens ambayo ilitwaa ubingwa huo katika mashindano ya kwanza yaliyofanyika Jinja, Uganda mwaka juzi ilienda mapumziko ikiwa na mabao 3-0.

  Nahodha Asha Rashid 'Mwalala' leo ameyefunga mabao mawili Queens ikishinda 4-1 

  Mabao ya Kilimanjaro Quuens katika mechi ya leo yamefungwa na Donisia Daniel, Asha Hamza na nahodha Asha Rashid " Mwalala" aliyefunga mawili wakati bao pekee la Uganda lilifungwa na Shadya Nankya katika dakika za lala salama.
  Kocha wa Kilimanjaro Queens, Bakari Shime alisema amefurahishwa na matokeo ya jana na anaamini wachezaji wake wataendelea na kasi walioionyesha ili kumaliza katika nafasi nzuri.
  Shime alisema michuano ya mwaka huu imekuwa na ushindani zaidi kwa sababu timu zote zilijiandaa kushindana kutokana na kuahirishwa kwa michuano hiyo ambayo awali ilipangwa kufanyika Mei mwaka huu.
  Kilimanjaro Queen itacheza mechi yake ya mwisho ya mashindano hayo Ijumaa dhidi ya Ethiopia wakati wenye Rwanda maarufu kwa jina la She- Amavubi watachuana na Kenya na timu itakayokuwa na pointi ndio itatangazwa kuwa mabingwa wapya.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KILIMANJARO QUEENS YAZINDUKA KOMBE LA CHALLENGE, YAICHAPA UGANDA 4-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top