• HABARI MPYA

  Jumatatu, Julai 23, 2018

  TFF YASHANGAA KLABU ZAO HADI SASA HAZIJAFANYA USAJILI NA DIRISHA LINAFUNGWA ALHAMISI

  Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limezikumbusha klabu za Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili ambazo hazijafanya usajili kupitia mfumo wa usajili wa TFF FIFA Connect kufanya hivyo haraka.
  Taarifa ya TFF kwa vyombo vya Habari leo imesema kwamba klabu ambazo bado hazijafanya usajili wawasiliane na TFF kama kuna msaada wowote wanahitaji ili kukamilisha usajili wao.
  TFF imesema dirisha la usajili litafungwa Alhamisi ya Julai 26, mwaka huu 2018 na TFF inasisitiza hakutakuwa na muda wa ziada katika usajili.
  Timu ambayo itashindwa kukamilisha usajili haitaruhusiwa kushiriki Ligi ya msimu ujao wa 2019/2019.

  Vilabu ambavyo havijafanya usajili mpaka sasa; Ruvu Shooting, Mbeya City, Tanzania Prisons, Mtibwa Sugar, Mwadui, Kagera Sugar, Alliance, Lipuli, African Lyon, KMC na Azam kwa upande wa Ligi Kuu.
  Ashanti United, Boma FC, Friends Rangers, Green Warriors, Kiluvya United, Majimaji FC, Mashujaa FC, Mawenzi Market, Mbeya Kwanza, Mgambo Shooting, Njombe Mji, Pamba FC, Dar City na Polisi Tanzania kwa upande wa Daraja la Kwanza.
  Area C United, Changanyikeni, Cosmopolitan FC, Kumuyange FC, Gipco FC, Mirambo FC, Madini FC, Mkamba Rangers, Mvuvumwa, Polisi Dar, The Mighty Elephant, Toto African, Villa Squad, Majimaji Rangers, Mtwivila City, Kasulu Red Star na Sahare All Stars kwa Daraja la Pili.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TFF YASHANGAA KLABU ZAO HADI SASA HAZIJAFANYA USAJILI NA DIRISHA LINAFUNGWA ALHAMISI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top