• HABARI MPYA

  Jumatatu, Julai 23, 2018

  SINGIDA UNITED WAMUACHIA ‘FEI TOTO’ ACHEZEE YANGA LAKINI AKIFELI JANGWANI AKAJARIBU NA NAMFUA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KLABU ya Singida United imeliandikia barua Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuliarifu juu ya kumuondoa kiungo Feisal Salum ‘Fei Toto’ katika usajili wake na kumuacha achezee wapinzani wao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Yanga SC.
  Barua ya SU inayotumia Uwanja wa Namfua, kwenda TFF iliyosainiwa na Katibu Mkuu, Abdulrahman Sima kwenda TFF imesema kwamba wamefikia uamuzi huo baada ya agizo la Mlezi wa timu, Mheshimiwa Dk. Mwigulu Nchemba, Mbunge wa Iramba Magharibi.
  “Dk Mwigulu amesema hakuna mgogoro wa kiusajili kwani alitoa ridhaa kwa mchezaji kwenda kujisajili na alikubaliana na viongozi wa Yanga wafanye na kwamba hakuna fedha inayorudishwa bali usajili huo ni mchango wake kwa klabu kwa makubaliano kwamba kama mchezaji hatakuwa na kiwango cha kubaki Yanga ataletwa Singida United,”amesema Sima.
  Feisal Salum ‘Fei Toto’ wameruhusiwa na Singida United kuchezea Yanga msimu ujao 

  Mapema mwezi huu Fei Toto alizua sintofahamu baada ya kutambulishwa na klabu mbili katika siku moja, asubuhi Singida United na jioni Yanga, wote wakisema wamemsaini kwa mkataba wa miaka mitatu kutoka JKU ya Zanzibar.
  Lakini sasa SU inaamua kurahisisha mambo kwa kumuacha kiungo huyo ‘nyondenyonde’ awatumikie wana Jangwani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SINGIDA UNITED WAMUACHIA ‘FEI TOTO’ ACHEZEE YANGA LAKINI AKIFELI JANGWANI AKAJARIBU NA NAMFUA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top