| Kipa wa Azam FC, Mwadini Ali akipangua mpira kwenye mazoezi ya timu hiyo juzi Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam huku kipa mpya wa timu hiyo, Ivo Mapunda akimshuhudia. Azam FC inajiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Jumamosi dhidi ya Simba SC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Hapa anakosekana kipa namba moja, Aishi Manula ambaye hayupo pichani, lakini walinda mlango wote hao watatu wako fiti kuelekea mchezo huo na ni uamuzi wa kocha Muingereza Stewart John Hall amuanzishe nani siku hiyo. |
0 comments:
Post a Comment