• HABARI MPYA

  Jumatano, Desemba 23, 2015

  PAUL NONGA AFUNGUA AKAUNTI YA MABAO YANGA IKIITANDIKA FRIENDS RANGERS 4-2

  MSHAMBULIAJI mpya wa Yanga SC, Paul Nonga (pichani kulia) amefunga mabao mawili leo asubuhi timu yake ikiibuka na ushindi wa 4-2 katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Friends Rangers Uwanja wa Boko, Dar es Salaam.
  Nonga aliyejiunga na Yanga SC mwezi huu katika dirisha dogo la usajili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanznaia Bara akitokea Mwadui FC ya Shinyanga amekuwa na mwanzo mzuri katika mchezo wake wa kwanza leo.
  Mabao mengine ya Yanga SC leo yamefungwa na kiungo Mzimbabwe, Thabani Kasumoko na mshambuliaji Mzanzibari, Matheo Anthony, wakati ya Friends Rangers yamefungwa na Freddy Cosmas Lewis na Khalid Badra.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: PAUL NONGA AFUNGUA AKAUNTI YA MABAO YANGA IKIITANDIKA FRIENDS RANGERS 4-2 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top