• HABARI MPYA

  Alhamisi, Desemba 24, 2015

  YAMETIMIA, SAMATTA SASA WA ULAYA… KUSAINI MIAKA MINNE NA NUSU GENK YA UBELGIJI

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta atasaini Mkataba wa miaka minne na nusu kujiunga na KRC Genk ya Ubelgiji. 
  Hiyo inafuatia makubalino yaliyofikiwa baina ya klabu hiyo ya Ubelgiji na timu ya sasa ya Samatta, TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
  Rais wa Mazembe, Moise Katumbi alikuwa Ubelgiji na inaelezwa amefikia makubalino na klabu hiyo na kinachosubiriwa ni mchezaji kwenda kusaini wakati wowote kuanzia sasa.
  Samatta ambaye aliibuka mfungaji bora wa Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kufunga mara nane, anaondoka Lubumbashi baada ya kuiwezesha Mazembe kutwaa Kombe la Afrika kwa mara ya tano.
  Mbwana Samatta (kushoto) sasa anahamia Ubelgiji kucheza soka ya kulipwa 

  Kwa mujibu gazeti la L’Equipe la Ufaransa, Mazembe na Genk wamefikia makubaliano ya biashara ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23.
  Kwa sasa, KRC Genk inashika nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Ubelgiji, maarufu kama Jupiler League, ikiwa imeshinda mechi nane, sare nne na kufungwa mara nane.
  Samatta alijiunga na Mazembe mwaka 2012 akitokea Simba SC ya Dar es Salaam, ambayo aliichezea kwa msimu mmoja tu baada ya kujiunga nayo akitokea African Lyon, zamani Mbagala Market.
  Samatta akiichezea Mazembe katika Klabu Bingwa ya Dunia mwezi huu nchini Japan
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YAMETIMIA, SAMATTA SASA WA ULAYA… KUSAINI MIAKA MINNE NA NUSU GENK YA UBELGIJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top