• HABARI MPYA

  Thursday, December 31, 2015

  MICHO AMJUMUISHA KIIZA KIKOSI CHA UGANDA MICHUANO YA CHAN 2016

  KOCHA wa timu ya taifa ya Uganda, 'The Cranes' Mseribia Milutin Sredojevic 'Micho' ametaja kikosi cha Michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN), akimjumuisha kiungo wa SC Villa 'Jogoo', Martin Kiiza.
  Micho, kocha wa zamani wa Yanga SC anatarajiwa kukutana na wachezaji wote 30 aliowaita katika kikosi cha awali Uwanja wa Nakivubo Kampala kwa mazoezi ya Jumamosi na Jumapili kabla ya kuwachuja na kubaki 23, ambao ataingia kambini Njeru kuanzia Januari 5 hadi 17 watakapokwenda Rwanda.
  Korongo wa Uganda amepangwa Kundi D pamoja Mali watakaocheza nao Januari 19, Zambia Januari 23 na Zimbabwe Januari 27 huko Rubavu.
  Kocha wa Uganda Milutin Sredojevic 'Micho' ametaja kikosi cha CHAN 2016

  Kikosi cha awali alichotaja Micho kinaundwa na makipa; Alitho James (Vipers) na Kisembo Douglas (Police FC)
  Mabeki: Nsubuga Joseph (Bright Stars), Bukenya Deus (Vipers), Muleme Isaac (SC Villa Jogoo), Waibi Yeseri (SC Villa Jogoo),  Hassan Wasswa Dazzo (KCCA), Shafik Bakaki (Vipers), Ibrahim Kiyemba (Lweza), Ibrahim Kiiza (Express FC), Sadat Kyambadde (Police), Timothy Musinguzi (Soana), Timothy Awany (KCCA).
  Viungo: Ambrose Kirya (SC Villa Jogoo), Keziron Kizito (Vipers), Rahmat Senfuka (Police), Basoma Andrew (Sadolin), Francis Olaki (Soana), Tony Odour (Express), Milton Karisa (BUL), Mike Ndera (BUL), Faruku Kawooya (SCVU) na Martin Kiiza (SC Villa Jogoo).
  Na washambuliaji ni Robert Ssentongo (URA), Geoffrey Sserunkuma (Lweza), Kalanda Frank (URA), Ndugwa Karim (SC Villa Jogoo), Lubega Edris (Proline) Nelson Senkatuka (KCCA) na Richard Wandyaka (JMC).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MICHO AMJUMUISHA KIIZA KIKOSI CHA UGANDA MICHUANO YA CHAN 2016 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top