• HABARI MPYA

  Alhamisi, Desemba 17, 2015

  AUBAMEYANG AZIDI KUJITENGENEZEA MAZINGIRA MWANASOKA BORA AFRIKA

  MSHAMBULIAJI Pierre-Emerick Aubameyang amefunga dakika ya 61 jana na kuipa Borrusia Dortmund ushindi wa 2-0 katika Robo Fainali ya Kombe la Ujerumani dhidi ya Augsburg, bao lingine likifungwa na Henrikh Mkhitaryan dakika ya 62 Uwanja wa WWK Arena.
  Nyota huyo wa Gabon, Aubameyang amefikisha mabao 18 msimu huu katika 16 Ujerumani na anazidi kuwa mpinzani mkuu wa Yaya Toure katika tuzo ya Mwanasoka Bora Afrika mwaka huu.

  Nyota wa Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang akishangilia jana baada ya kuifungia Borussia Dortmund dhidi ya Augsburg  PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Aubameyang ameingia katika orodha ya mwisho ya wachezaji watatu kuwania tuzo ya Mwanasoka Bora wa Jumla wa Afrika pamoja na Andre Ayew wa Ghana na Swansea City na Yaya Toure wa Ivory Coast na Manchester City, anayeshikilia tuzo hiyo.
  Mshindi apatikana kutokana na kura zitakazopigwa na makocha wakuu wa timu za taifa au Wakurugenzi wa Ufundi wa Vyama na mashirikisho ya soka ya nchi zote wanachama wa CAF.
  Upande wa tuzo ya Mwanasoka Bora Anayecheza Afrika, mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta ameingia tatu bora pamoja na kipa Robert Kidiaba anayecheza naye TP Mazembe ya DRC na Baghdad Boundjah wa Algeria na Etoile du Sahel ya Tunisa. 
  Washindi wote wa tuzo hizo za Shirikisho la Soka Afrika (CAF) watatangazwa katika usiku wa tuzo za Glo-CAF Januari 7 mwaka 2016 mjini Abuja, Nigeria.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AUBAMEYANG AZIDI KUJITENGENEZEA MAZINGIRA MWANASOKA BORA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top