• HABARI MPYA

    Thursday, December 24, 2015

    REDONDO RUKSA KUICHEZEA MBEYA CITY DHIDI YA YANGA SC JUMAMOSI TAIFA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    WACHEZAJI Tumba Swedi na Ramadhani Chombo 'Redondo' wameidhinishwa kuchezea klabu ya Mbeya City FC ya Mbeya katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
    Redondo anayeungana tena na Juma Kaseja, Haruna Shamte, Juma Nyosso na Haruna Moshi 'Boban' aliocheza nao Simba SC awali, sasa atacheza dhidi ya Yanga SC Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 
    Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji chini ya Mwenyekiti wake Richard Sinamtwa, jana Jumatano ilikaa na kupitia malalamiko/pingamizi za usajili wa wachezaji yaliyokuwa yamewasilishwa TFF mara tu baada ya usajili wa dirisha dogo uliofungwa Disemba 15, mwaka huu.
    Kamati hiyo imeweza kupitia na kupitisha usajili kwa vilabu mbalimbali, huku pia kamati hiyo ikizuia baadhi ya usajili wa wachezaji waliosajiliwa, mpaka pande hizo mbili zitakapomalizana ndipo mchezaji husika ataweza kuitumikia klabu yake mpya.
    Ramadhani Chombo 'Redondo' sasa atacheza dhidi ya Yanga SC Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

    TAARIFA KAMILI YA KAMATI YA SHERIA NA HADHI ZA WACHEZAJI

    A. USAJILI
    1. Kamati imepitisha usajili wa wachezaji walioombewa kwa vilabu vifuatavyo vya ligi kuu

    1. AZAM FC - mchezaji mmoja 
    Ivo Philiph Mapunda (huru)

    2. COASTAL UNION- wachezaji watatu
    i. Omary Wayne Maunda-Mkopo toka Azam
    ii. Miraji Adam Seleman-mkopo toka Simba
    iii. Ramadhani Ali Thabit-huru

    3. MGAMBO SHOOTING
    i. Mudathir M. Khamis-Yanga
    ii. Nurdin Mkomeni-huru
    iii. Godson Mmasa-alikuwa mchezaji wa Mgambo, wameomba kumsajili tena

    4. MTIBWA SUGAR
    i. Alex Mwambisi-huru
    ii. Boniface Maganga-Mkopo kutoka Simba
    iii. Kelvin Iddi Friday-Mkopo kutoka Azam
    iv. Abdallah Said Makangana-alisahaulika usajili uliopita ni mchezaji anayendelea

    5. MWADUI SC
    i. Abdallah Mfuko-huru
    ii. Ismail Gambo-Mkopo kutoka Azam FC

    6. NDANDA SC
    i. Braison Raphael-Mkopo kutoka Azam
    ii. Jackson John Nkwera-Sinza Srtars

    7. MBEYA CITY
    i. Ramadhani Selemani Chombo-huru
    ii. Abdallah Salum Juma-Toto Africans
    iii. Deogratius Julius-Kagera Sugar

    8. TANZANIA PRISONS
    i. Baraka Majogoro-Wenda FC

    9. TOTO AFRICANS
    i. Shija Hassan Mkina-huru
    ii. Frank B Kimati-huru
    iii. Ladslaus Mbogo-huru
    iv. Yusuf Seleman Mpili-huru
    v. Maneno Steven Shaban-huru

    10. SIMBA SC
    i. Kiongera Raphael-Amerudishwa toka KCB alikokuwa anacheza kwa mkopo
    ii. Novaty Lufunga-African Sports
    iii. Haji Mohamed Ugando-Jaki Academy
    iv. Brian Majegwa-Azam FC

    11. STAND UNITED
     i. Assouman N’gueassan David-FC Olympic Sports Abobo

    12. YANGA SC
    i. Issoufou Boubacar-
    ii. Paul Nonga-Mwadui

    13. JKT RUVU
    i. Waziri Shaban Iddi-huru
    ii. Hamis Thabit-African Lyon
    iii. Hassan Dilunga- Stand United

    14. MAJIMAJI
     i. Kennedy Stainley Kipepe-Njombe Mji
    ii. Abubakar B Bakari-huru
    iii. Sixmund Ally Mwakasekaga-huru
    iv. Paulo Maona Terry-huru

    15. KAGERA SUGAR
    i. Ramadhani Mzee Kipalamoto- Kagera Sugar
    ii. Samwel Donald Ngassa-huru
    iii. Shaaban Ibrahim Sunza-Mshikamano
    iv. Martin Lupart Mlolere-Abajalo, Dar es Salaam
    v. Juma Jabu Hamis-huru

    16. AFRICAN SPORTS
    i. Hamis Twairu Juma-U20, huru
    ii. Hamad Nathaniel Mbumba-Polisi Tabora
    iii. Hamad Nathaniel Mbumba-African Lyon
    iv. Charles Martin Ilamfya-Mkopo toka Mtibwa
    v. Rajab Isihaka-huru
    vi. Reyna Mgungira-huru

    USAJILI UFUATAO UMEZUILIWA KWA MAELEZO YAFUATAYYO

    1. AFRICAN SPORTS
    i. Karim Hamud Juma aliyeombea kusajiliwa na African Sports akitokea PolisiTabora usajili wake
    ii. Michael Victor Mgimwa kamati imezuia usajili wake mpaka hati ya uhamisho wa kimataifa umezuiwa mpaka timu mbili zitakapofikia makubaliano itakapotumwa toka Thailand, mchezaji huyu alikuwa anaitumikia Rio United ya Thailand.

    2. MAJIMAJI SPORTS CLUB
    i. Danny David Mrwanda na Lulanga Andrew Mapunda-kamati imezuia usajili wake mpaka vilabu viwili vya Majimaji inayotaka kumsajili na Lipuli iliyokuwa inawamiliki wachezaji hao zitakapokubaliana na kutuma kwa maandishi makubaliano yao TFF.

    3. MBEYA CITY
    i. Kamati baada ya uchunguzi imejiridhisha kwamba mchezaji Tumba Sued aliyewekewa pingamizi na Coastal Union alisaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu na Coastal Union siku ya tarehe 12 June, 2014 na mkataba huu ulienda kushuhudiwa kwa mwanasheria siku ya tarehe 23 Agosti 2014, kushuhudiwa huku hakukubatilisha mkataba uliosainiwa tarehe 12 June 2014.
    Hivyo kamati inamtangaza Tumba Sued kuwa mchezaji huru toka tarehe 11 Desemba na kwa sasa ni mchezaji halali na amepitishwa kuichezea Mbeya City ya Mbeya.
    ii. Kamati pia inatoa onyo kali kwa klabu ya Mbeya City na imeagiza kesi hii ipelekwe kwenye kamati ya nidhamu kwa kuongea na mchezaji Ditram Nchimbi ambaye ni mchezaji halali wa Majimaji ya Songea ambaye alisaini mkataba wa miaka miwili na Majimaji  tarehe 20 Oktoba 2014 hivyo mkataba wake utaisha tarehe 19 Octoba 2016. Mbeya City wameongea na mchezaji mwenye mkataba uliozidi miezi 6 bila kuomba ridhaa ya klabu inayommiliki ambayo ni Majimaji.

    4. JKT RUVU
    JKT Ruvu iliomba kumsajili mchezaji Hassan Dilunga kutoka Stand United kwa kufata taratibu zote ikiwa ni pamoja na kuongea na klabu yake ya Stand United na kupata kibali cha kumsajili Dilunga kutoka kwa uongozi halali wa Stand United kupitia kwa mwenyekiti na katibu wa Stand United. Pamoja na ruhusa kutoka kwa Stand United bado kuna mtu anayeitwa mratibu wa Stand United aliiandikia barua TFF akipinga usajili wa mchezaji huyu.
    Kamati imesikitishwa na kitendo cha mtu huyu ambaye hatambuliki na TFF na wala siyo mtu anayepaswa kuwasiliana na TFF kwa kuingilia maamuzi ya viongozi halali wa Stand United na imeamuru mtu huyo anayeitwa Mbasha Matutu apelekwe kamati ya maadili kwa kupora mawasiliano ya Stand United wakati viongozi halali wanaotambulika kikatiba wa Stand United wapo.
    Kamati imeamua mratibu Mbasha Matutu apelekwe kamati ya maadili kufuatia kutofata na kuheshimu uongozi halali wa klabu ya Stand United.

    5. NDANDA SC-RAMADHANI KIPALAMOTO
    Ndanda SC ilileta maombi ya kumsajili mchezaji Ramadhani Salim Kipalamoto amabye alikuwa anachezea Abajalo SC ya Dar es Salaam, maombi haya yamekataliwa kwa kuwa mchezaji husika alikuwa pia ameombewa kusajiliwa na Kagera Sugar na klabu yake ya Abajalo ikatoa ridhaa ya mchezaji huyu kwenda Kagera Sugar ya mkoani Kagera.

    6. NDANDA SC-IBRAHIM IS-HAAK
    Kamati ya Sheria na hadhi za wachezaji  imeridhia ombi la mchezaji Ibrahim Is-haki aliyedai klabu yake ya Ndanda SC kuvunja mkataba wake kwa kutomlipa hela yake ya usajili kama walivyokubaliana.
    Mchezaji huyu amevunja mkataba wake baada ya maombi yake TFF kukubaliwa na mwakilishi wa klabu yake ya Ndanda SC, Edmund Njowoke ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Ndanda SC, na kamati imeridhia maombi ya timu ya Geita SC ya kutaka kumsajili.
    Mchezaji Ibrahim Is-haak amepitishwa kuichezea timu ya Geita Gold SC ya Geita.

    7. MWADUI SC
    Kamati imeridhia pingamizi la klabu ya KMC ya Kinondoni kumzuia mchezaji Emmanuel Memba aliyeombewa kusajiliwa na Mwadui Sc kwa kutofata utaratibu. Kamati inaiagiza klabu ya Mwadui kuongea na KMC wamiliki wa mchezaji ili wawaruhusu kumtumia mchezaji husika.

    8. KIMONDO SC
    Klabu ya Kurugenzi ya Mafinga imeleta pingamizi dhidi ya Kimondo FC kwa kumsajili mchezaji wao George Mpole bila kufata utaratibu. Kamati inaishauri Kimondo SC kufata utaratibu wa usajili kwa kuongea na Kurugenzi.

    9. GEITA GOLD SC
    TFF imepokea ombi la pingamizi kutoka kwa timu ya Rhino Rangers kwa Geita Gold SC kumsajili mchezaji wao Pius Kisambale bila kufuata utaratibu. Geita inatakiwa kufuata utaratibu ikiwa ni pamoja na kuongea na uongozi wa timu ya Rhino SC ya Tabora

    10. POLISI MOROGORO
    Imeleta ombi la pingamizi la wachezaji wao wawili
    i. Anafi Selemani Ally
    ii. Mohamed Kapeta kusajiliwa na timu yoyote kwa kuwa ni wachezaji wao. Ombi la pingamizi kwa wachezaji hao limekubaliwa na kamati.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: REDONDO RUKSA KUICHEZEA MBEYA CITY DHIDI YA YANGA SC JUMAMOSI TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top