• HABARI MPYA

  Sunday, December 27, 2015

  AZAM FC YAZIDI KUNG’ARA LIGI KUU, YAITANDIKA KAGERA SUGAR 2-0, TOTO YALALA 1-0 NYUMBANI

  MATOKEO NA RATIBA LIGI KUU YA VODACOM TZ BARA
  Leo; Desemba 27, 2015
  Azam FC 2-0 Kagera Sugar
  Toto Africans 0-1 African Sports
  Jana; Desemba 26, 2015
  Ndanda FC 1 - 3 JKT Ruvu
  Yanga SC 3 - 0 Mbeya City
  Majimaji 0 - 2 Prisons
  Mwadui FC 1 - 1 Simba SC
  Mtibwa Sugar 3 - 0 Mgambo JKT
  Coastal Union 1 - 3 Stand United
  MECHI ZIJAZO;
  Desemba 30, 2015
  Azam FC vs Mtibwa Sugar
  Januari 1, 2015
  Ndanda FC vs Simba SC
  Shomary Kapombe wa Azam FC (katikati) akikimbia baada ya kuifungia timu yae bao a pili, huku kipa wa Kagera Sugar, Agathon Anthony akiwa anashuhudia mpira ukitinga nyavuni 

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  AZAM FC imeendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya jioni ya leo kuifunga Kagera Sugar mabao 2-0 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Ushindi huo, unaifanya timu hiyo ya Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake ifikishe pointi 32 baada ya kucheza mechi 12, ikizidiwa pointi moja na mabingwa watetezi, Yanga SC wenye mchezo mmoja zaidi.
  Mabao ya mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati leo yamefungwa na mshambuliaji kutoka Ivory Coast, Kipre Herman Tchetche na beki mzalendo, Shomary Salum Kapombe.
  Tchetche alifunga bao la kwanza kwa kichwa dakika ya tisa, akimalizia kona maridadi iliyochongwa na kiungo Himid Mao Mkami ‘Ninja’.
  Kipa Aishi Manula alicheza kwa mguu mkwaju wa penalti wa Nahodha wa Kagera Sugar, Salum Kanoni Kupela dakika ya 35, baada ya beki Msenegali, Racine Diouf kumuangusha Ramadhani Kiparamoto kwenye eneo la hatari.
  Kapombe aliifungia Azam FC bao la pili dakika 74 baada ya kupasua katikati ya mabeki wa Kagera kufuatia kutanguliziwa pasi nzuri na Himid Mao.
  Mchezo mwingine wa Ligi Kuu leo, Toto African imefungwa 1-0 nyumbani na African Sports ya Tanga Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.
  Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Aishi Manula, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni/Abdallah Kheri dk34, Serge Wawa, Kipre Bolou/Ramadhani Singano ‘Messi’, Racine Diouf, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Himid Mao, Kipre Tchetche, John Bocco/Farid Mussa dk46 na Didier Kavumbangu. 
  Kagera Sugar: Antony Agaton, Salum Kanon, Juma Jabu, Erick Kyaruzi, Shaban Ibrahim, Mbaraka Yusuph, Daud Jumanne, Martim Lupart, Ramadham Kiparamoto na Pauj Ngwai/Adam Kingwande dk58.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAZIDI KUNG’ARA LIGI KUU, YAITANDIKA KAGERA SUGAR 2-0, TOTO YALALA 1-0 NYUMBANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top