• HABARI MPYA

  Jumatano, Desemba 23, 2015

  HIDDINK AMPANDISHA CHELSEA A KINDA MZAMBIA ALIYEZINGUANA NA FABREGAS

  KINDA Mbelgiji wa Chelsea mwenye asili ya Zambia, Charly Musonda amepandishwa kikosi cha kwanza siku chache baada ya 'kuzinguana' na Cesc Fabregas mazoezini.
  Musonda, ambaye anatakiwa na timu kadhaa kwa mkopo mwezi ujao, alikuwa kivutio katika mchezo wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka ya Chelsea dhidi ya Middlesbrough Jumatatu usiku.
  Kiwango chake kitamsaidia kuingia kwenye mipango ya kocha mpya wa muda, Guus Hiddink kati ya sasa na mwishoni mwa msimu.
  Charly Musonda amepandishwa kikosi cha kwanza cha Chelsea na kocha Hiddink

  CHARLY MUSONDA NI NANI?

  Kuzaliwa: Oktoba 15, 1996
  Alipozaliwa: Brussels, Ubelgiji
  Nafasi: Kiungo mshambuliaji
  Klabu ya awali: Anderlecht
  Timu za Taifa
  Timu za vijana chini ya umri wa miaka 17, 18, 19 na 21 za Ubelgiji 
  Musonda ambaye ni kiungo mshambuliaji, wiki iliyopita alizinguana na mchezaji mkongwe wa klabu hiyo, Fabregas mazoezini.
  Kiungo wa kimataifa wa Hispania, alikasirika baada ya Musonda kuupitia mpira kichwani mwake.
  Fabregas akalipiza kwa kumchezea 'kindava' kinda huyo wa umri wa miaka 19 jambo ambalo liliwashangaza wachezaji wengine.
  Tukio hilo lilitokea katika siku za mwisho za kocha Mreno Jose Mourinho viwanja vya mazoezini ya klabu, eneo la Cobham.
  Musonda ni mtoto wa kiungo wa kimataifa wa Zambia na klabu ya Anderlecht, Charly Musonda Snr. 
  Kocha Hiddink amemjumuisha Musonda wa pili kutoka kushoto katika mazoezi ya kikosi cha kwanza Chelsea
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: HIDDINK AMPANDISHA CHELSEA A KINDA MZAMBIA ALIYEZINGUANA NA FABREGAS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top