• HABARI MPYA

  Alhamisi, Desemba 31, 2015

  MAN UNITED 'WAENDEA MBIO' SAINI YA KIUNGO MBRAZIL WA LAZIO

  KLABU ya Manchester United ipo kwenye mazungumzo ya kumsajili kiungo Lazio, Felipe Anderson katika jitihada zake za kusaka kiungo mbunifu.
  Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 22 alitakiwa na kocha Louis van Gaal tangu mwanzoni mwa msimu na wasaka vipaji wa Old Trafford wameendelea kufuatilia maendeleo yake mjini Rome, huku Lazio ikimthaminisha kwa Pauni Milioni 35.
  United bado inafanya mpango wa kumsajili Sadio Mane - ambao ulikwama Agosti - na Southampton haiko tayari kumuuza mmoja wa wachezaji wake tegemeo Januari.

  Manchester United inataka saini ya kiungo wa Lazio, Felipe Anderson ifikapo Januari PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Anderson, ambaye amefunga mabao matano msimu huu kutoka eneo la kiungo, amezivutia klabu nyingine kadhaa kubwa Ulaya.
  United imejikuta katika wakati mgumu msimu huu kutokana na kukosa kiungo wa maana na inajipanga kuimarisha kikosi chake kabla ya kuanza mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya England.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAN UNITED 'WAENDEA MBIO' SAINI YA KIUNGO MBRAZIL WA LAZIO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top