• HABARI MPYA

  Ijumaa, Desemba 18, 2015

  RONALDO AANZA MIKAKATI YA MAISHA BAADA YA SOKA, KUFUNGUA HOTELI NNE 'ZA HATARI' DUNIANI

  MWANASOKA bora wa dunia, Cristiano Ronaldo tayari ameanza kufikiria maisha yake ya baadaye baada ya kusema hawezi kuwa mchezaji nyota wa Real Madrid daima.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 anatarajiwa kuondoka Real mwishoni mwa msimu huu na ana mipango mikubwa kwa ajili ya maisha yake ya baadaye akikiri kwamba; "Maisha hayatakuwa hivi daima,".
  Alhamisi, Ronaldo alizundua mpango mkubwa usio wa soka ambao tayari ni mradi wa Pauni Milioni 54 wa kufungua hoteli tatu za 'CR7' katika miji yenye uhusiano na maisha yake: Funchal, Lisbon na Madrid – na mwingine ambao unahusishwa na maisha yake ni New York ambako anatarajiwa kuhamia.
  Cristiano Ronaldo akifurahi wakati wa uzinduzi wa mradi wa hoteli za CR7 mjini Lisbon, Ureno jana PICHA ZAIDI GONGA HAPA


  Na nyota huyo wa Ureno ameweka wazi kwamba uhusiano wa kibiashara na kampuni ya Pestana Hotel Group ya kwao, Ureno ndiyo hatua inayofuata katika kuandaa maisha yake baada ya soka.
  "Kazi yangu ni kucheza soka, lakini maisha hayatakuwa kama hivi daima,"amesema Ronaldo. "Natakiwa kuelekeza nguvu zangu kwenye huu mradi mpya na nina timu nzuri inayonizunguka duniani.
  "Mimi ni mdogo, lakini najihisi shwari sana, hivyo huu mradi ni wa kuvutia kwangu. Nafikiria mustakabali wangu, na mwanangu na familia yangu.
  Mapema Ronaldo alipoza uvumi kwamba wa kuhamia Paris Saint-Germain mwishoni mwa msimu kwa kusema kwamba anapenda zaidi kuwa katika Jiji la Madrid. Jiji kuu la Ufaransa si moja ya maeneo ambayo amelenga kwa maisha yake ya baadaye.
  Hoteli ya kwanza itafunguliwa mwakani mjini Madeira, ambako Ronaldo alizaliwa. Itafuatiwa na hoteli ya Lisbon mwishoni mwa mwaka 2016 ambako alikwenda akiwa kinda kuchezea klabu ya Sporting Lisbon. Hoteli ya Madrid inatarajiwa kufunguliwa mwaka 2017.
  Akitania kuhusu mradi wake huo, Ronaldo alicheka akisema; "Nitakuwa makini na vitanda vyangu!'
  Cristiano Ronaldo (left) poses with Dionisio Pestana, owner of the Pestana Hotel Group, in Lisbon on Thursday
  Cristiano Ronaldo (kushoto) akiwa na Dionisio Pestana, mmiliki wa kampuni ya Pestana Hotel Group mjini Lisbon jana

  Winga huyo wa zamani wa Manchester United hajaelezea kuhusu uwekezaji wa mradi wake huo England, ingawa kuna hoteli itafunguliwa New York mwaka 2017.
  Awali alielezea nia yake ya kwenda kumalizia soka yake katika Ligi Kuu ya Marekani (MLS) na kuingia ubia wa kibiashara na Big Apple baada ya kununua jengo lenye thamani ya Pauni Milioni 11.1 mapema mwaka huu kwamba inaweza kumfanya siku achezee ama New York City au New York Red Bulls.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: RONALDO AANZA MIKAKATI YA MAISHA BAADA YA SOKA, KUFUNGUA HOTELI NNE 'ZA HATARI' DUNIANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top