• HABARI MPYA

  Jumatano, Desemba 16, 2015

  RIVER PLATE YATANGULIA FAINALI, MAZEMBE YAAGA MIKONO MITUPU KOMBE LA DUNIA

  TIMU ya River Plate ya Argentina imetinga fainali ya Klabu Bingwa ya Dunia nchini Japan 2015, baada ya kuwachapa bao 1-0 wenyeji, Sanfrecce Hiroshima Uwanja wa Nagai mjini Osaka.
  Shukrani kwake, Lucas Alario aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 72 na sasa wababe hao wa Argentina watakutana na mshindi wa Nusu Fainali ya pili kesho, kati ya mabingwa wa Ulaya, Barcelona dhidi ya Guanzghou Evergrande, mabingwa wa Japan.

  Katika mchezo uliotangulia kusaka nafasi ya tano, Club America imeifunga TP Mazembe ya DRC mabao 2-1.

  Osvaldo Martinez wa Club America (kushoto) akigombea mpira na Boudacar Diarra wa TP Mazembe (kulia) 

  Mabao ya Club America yamefungwa na washambuliaji Dario Benedetto na Martin Zuniga, wakati bao pekee la wawakilishi wa Afrika limefungwa na Rainford Kalaba.
  Washambuliaji wote wa kimataifa wa Tanzania walianza katika mchezo wa leo, Mbwana Samatta akimaliza dakika 90, wakati Thomas Ulimwengu alimpisha Roger Assale dakika ya 72. 
  Kikosi cha Ignacio Ambriz kiliingia katika mchezo huo baada ya kipigo cha dakika ya mwisho cha Guangzhou Evergrande katika Robo Fainali, wakati vijana wa Patrice Carteron kutoka Lubumbashi waliingia katika mchezo huo baada ya kuchapwa mabao 3-0 na Sanfrecce Hiroshima.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: RIVER PLATE YATANGULIA FAINALI, MAZEMBE YAAGA MIKONO MITUPU KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top