• HABARI MPYA

  Alhamisi, Desemba 17, 2015

  YANGA SC YAMSIMAMISHA NIYONZIMA NA KUMKATA MSHAHARA

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  KIUNGO wa Yanga SC, Haruna Hakizimana Fadhil Niyonzima atapokea nusu mshahara kwa muda usiojulikana, baada ya kusimamishwa na uongozi wa klabu hiyo kwa utovu wa nidhamu.
  Katibu Mkuu wa Yanga SC, Dk. Jonas Tiboroha ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE kwamba klabu imemsimamisha Niyonzima kwa muda usiojulikana baada ya kurudia kuchelewa kujiunga timu kufuatia ruhusa maalum.
  Dk Tiboroha amesema uamuzi huo umefikiwa na kikao cha Kamati ya Mashindano, chini ya Mwenyekiti wake, Isaac Chanji jana mjini Dar es Salaam.

  Haruna Niyonzima atapokea nusu mshahara kwa muda usiojulikana, baada ya kusimamishwa na uongozi wa Yanga kwa utovu wa nidhamu

  Na amesema hiyo imefuatia Niyonzima kushindwa kujirekebisha licha ya kuonywa mara kadhaa juu ya desturi hiyo isiyopendeza.
  Niyonzima aliibuka mapema wiki hii mjini Dar es Salaam na kujisalimisha klabuni akiwa amefungwa plasta gumu (PoP), maarufu kama ‘hogo’, baada ya Yanga SC kusema itamchukulia hatua za kinidhamu kwa kitendo cha kuchelewa kurejea katika timu.
  Nahodha huyo wa Rwanda aliruhusiwa kwenda kuichezea timu yake ya taifa katika Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge nchini Ethiopia, lakini baada ya mashindano akachelewa kurejea Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA SC YAMSIMAMISHA NIYONZIMA NA KUMKATA MSHAHARA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top