• HABARI MPYA

  Jumamosi, Desemba 19, 2015

  MAN UNITED TAABANI, YAKUNG’UTWA 2-1 NA NORWICH OLD TRAFFORD, CHELSEA YAZINDUKA

  MATOKEO LIGI KUU YA ENGLAND LEO
  Everton 2 - 3 Leicester City
  Man United 1 - 2 Norwich City
  Southampton         0 - 2 Tottenham Hotspur
  Stoke City 1 - 2 Crystal Palace
  Chelsea 3 - 1 Sunderland
  West Bromwich 1 - 2 Bournemouth
  Kocha Louis van Gaal sasa amekalia kuti kavu baada ya Manchester United kufungwa 2-1 nyumbani leo PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  KOCHA Mholanzi, Louis Van Gaal sasa anaangalia mlango wa kutokea Manchester United, baada ya timu hiyo kuchapwa mabao 2-1 nyumbani Uwanja wa Old Trafford na Norwich City.
  Walioizamisha United leo ni Cameron Jerome aliyefunga dakika ya 38 na Alexander Tettey aliyefunga dakika ya 54, wakati bao la kufutia machozi la Mashetani Wekundu limefungwa na United Anthony Martial dakika ya 66.
  Saa 48 baada ya kumfukuza kocha Mreno, Jose Mourinho, Chelsea imeibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya Sunderland Uwanja wa Stamford Bridge, London.

  Branislav Ivanovic akipongezwa na wachezaji wenzake wa Chelsea baada ya kufunga PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Mabao ya The Blues yamefungwa na Branislav Ivanovic dakika ya tano, Pedro Rodriguez Ledesma dakika ya 13 na Oscar dos Santos Emboaba Junior kwa penalti dakika ya 50, wakati bao la Sunderland limefungwa na Fabio Borini dakika ya 53.
  Leicester City imezidi kupaa kileleni mwa Ligi Kuu kufuatia usgindi wa 3-2 dhidi ya Everton Uwanja wa Goodison Park.
  Mualgeria Riyad Mahrez alifunga mabao mawili kwa penalti dakika ya 27 na 65, kabla ya Shinji Okazaki kufunga la tatu dakika ya 69, wakati mabao ya wenyeji yamefungwa na Romelu Lukaku dakika ya 32 na Kevin Mirallas dakika ya 89.
  Tottenham Hotspur imeshinda 2-0 ugenini dhidi ya Southampton, mabao ya Harry Kane dakika ya 40 na Bamidele Alli dakika ya 43 Uwanja wa St. Mary's.
  Crystal Palace imeshinda pia ugenini 2-1 dhidi ya Stoke City mabao yao yakifungwa na Connor Wickham kwa penalti dakika ya 46 na Chung-yong Lee dakika ya 88, wakati bao la wenyeji limefungwa na Bojan Krkic kwa penalti dakika ya 76.
  Bournemouth nao pia wameshinda ugenini 2-1 dhidi ya West Bromwich Albion mabao yao yakifungwa na Adam Smith dakika ya 52 na Charlie Daniels kwa penalti dakika ya 87, wakati la wenyeji limefungwa na Gareth McAuley dakika ya 79.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAN UNITED TAABANI, YAKUNG’UTWA 2-1 NA NORWICH OLD TRAFFORD, CHELSEA YAZINDUKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top