• HABARI MPYA

  Jumatatu, Desemba 28, 2015

  ARSENAL YAPAA KILELENI LIGI KUU ENGLAND, MAN UNITED NA CHELSEA ZATOKA SARE 0-0

  MATOKEO LIGI KUU YA ENGLAND LEO
  Desemba 28, 2015  
  Manchester United 0-0 Chelsea
  West Ham United 2-1 Southampton
  Arsenal 2-0 Bournemouth
  Everton 3-4 Stoke City
  Watford 1-2 Tottenham Hotspur
  Crystal Palace 0-0 Swansea City
  West Bromwich 1-0 Newcastle United
  Norwich City 2-0 Aston Villa
  MECHI ZIJAZO…
  Kesho Desemba 29, 2015
  Leicester City v Manchester (Saa 4:45 usiku)
  Desemba 30, 2015
  Sunderland v Liverpool (Saa 4:45 usiku)

  Mesut Ozil akishangilia baada ya kuifungia Arsenal bao la pili PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  ARSENAL imepanda kileleni mwa Ligi Kuu ya England kufuatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya 
  Bournemouth jioni ya leo Uwanja wa Emirates, London.
  Ushindi huo unawafanya Washika Bunduki hao wafikishe pointi 39, baada ya kucheza mechi 19, wakiizidi pointi moja tu Leicester City iliyocheza mechi 18.
  Mabao ya timu ya Arsene Wenger leo yamefungwa na Gabriel Armando de Abreu dakika ya 27 na Mesut Ozil dakika ya 63.
  Mchezo mwingine wa ligi hiyo leo, Manchester United imelazimishwa sare ya 0-0 na Chelsea Uwanja wa Old Trafford.

  Nemanja Matic alipoteza nafasi ya wazi ya kufunga akiwa amebaki na David de Gea akapaisha PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  West Ham United imeshinda 2-1 nyumbani dhidi ya Southampton, mabao yake yakifungwa na Michail Antonio dakika ya 69 na Andy Carroll dakika ya 79, wakati  Carl Jenkinson alijifunga dakika ya 13 Uwanja wa Boleyn Ground kuwapatia wageni bao la kuongoza.
  Stoke City imeshinda ugenini 4-3 dhidi ya Everton Uwanja wa Goodison Park, mabao yake yakifungwa na Xherdan Shaqiri dakika ya 16 na 45, Jose Luis Mato Sanmartin dakika ya 80 na Marko Arnautovic kwa penalti dakika ya 91. 
  Mabao ya Everton yamefungwa na Romelu Lukaku dakika ya 22 na 64 na Gerard Deulofeu dakika ya 71. Tottenham Hotspur imeshinda ugenini 2-1 dhidi ya Watford mabao yake yakifungwa na Erik Lamela dakika ya 17 na Heung-Min Son dakika ya 89, wakati la wenyeji limefungwa na Odion Ighalo dakika ya 41 Uwanja wa Vicarage Road.

  Nyota wa Tottenham Hotspur, Son Heung-min (kushoto) akishangilia baada ya kuifungia timu yake dakika ya 89 PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Crystal Palace imelazimishwa sare ya 0-0 na Swansea City Uwanja wa Selhurst Park, wakati West Bromwich Albion imeshinda 1-0 dhidi ya Newcastle United bao pekee la Darren Fletcher dakika ya 78 Uwanja wa The Hawthorns na Norwich City imeshinda 2-0 dhidi ya Aston Villa, mabao ya Jonny Howson dakika ya 24 na Dieudonne Mbokani Bezua dakika ya 87 Uwanja wa Carrow Road.
  Ligi Kuu inaendelea kesho, Leicester City wakiikaribisha Manchester City Uwanja wa King Power, wakati keshokutwa Sunderland watakuwa wenyeji wa Liverpool Uwanja wa Light.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ARSENAL YAPAA KILELENI LIGI KUU ENGLAND, MAN UNITED NA CHELSEA ZATOKA SARE 0-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top