• HABARI MPYA

  Saturday, December 19, 2015

  NGASSA ACHEZA KIPINDI KIMOJA, FREE STATE YASHINDA AFRIKA KUSINI

  KIUNGO mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mrisho Khalfan Ngassa amecheza kwa dakika 45 leo timu yake, Free State Stars ikiibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Jomo Cosmos katika mchezo wa Ligi Kuu ya ABSA Afrika Kusini Uwanja wa Goble Park mjini Bethlehem.
  Bao pekee la Free State leo limefungwa na Hendrik Somaeb dakika ya 60 aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya mchezaji wa zamani wa Yanga SC, Ngassa.
  Ngassa alianza kuonyesha dalili za kusikia maumivu tangu dakika ya 40 baada ya kugongan na kipa wa Cosmos, Sherwin Naicker na kipindi cha pili hakurudi uwanjani.
  Kikosi cha Stars kilikuwa; Diakite, Masehe, Mashego/Makhaela dk46, Chabalala, Shabalala, Thebekang, Ngassa/Somaeb dk46, Sekola, Jaftha/Vilakazi dk78), Kerspuy na Venter.
  Cosmos: Naicker, Nsabiyumva, Mngomezulu, Mthembu/Mntambo dk59, Sithole, Monare, Mhone, Jampies, Zulu, Mashumba/Mukamba dk59 na Aka.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NGASSA ACHEZA KIPINDI KIMOJA, FREE STATE YASHINDA AFRIKA KUSINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top