• HABARI MPYA

  Jumapili, Desemba 27, 2015

  ARSENAL YATANDIKWA RISASI NNE, CHELSEA YATOA SARE, LIVERPOOL YAIADABISHA LEICESTER, MAN UTD HADI HURUMA! YACHAPWA TENA 2-0

  MATOKEO MECHI ZA LIGI KUU YA ENGLAND JANA
  Southampton 4 - 0 Arsenal
  Newcastle United 0 - 1 Everton
  Chelsea 2 - 2 Watford
  Bournemouth 0 - 0 Crystal Palace
  Swansea City 1 - 0 West Bromwich Albion
  Tottenham Hotspur 3 - 0 Norwich City
  Manchester City 4 - 1 Sunderland
  Aston Villa 1 - 1 West Ham United
  Liverpool 1 - 0 Leicester City
  Stoke City 2 - 0 Manchester United
  Kiungo Mkenya wa Southampton, Victor Wanyama akimrukia mchezaji mwenzake Jose Fonte (katikati) na baada ya Martina kufunga jana dhidi ya Arsenal katika mchezo wa Ligi Kuu ya England PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  WASHIKA Bunduki, Arsenal wamepokonywa mtutu na Southampton na kutandikwa risasi nne jana Uwanja wa St Marry’s katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.
  Rhu-Endly Martina alianza kuiadhibu timu ya Arsene Wenger dakika ya 19, kabla ya Shane Long kufunga la pili dakika ya 55 na la nne dakika ya 92, wakati bao la tatu lilifungwa na Jose Fonte dakika 69.
  Everton imepata ushindi wa 1-0 ugenini dhidi ya Newcastle United, bao pekee la Tom Cleverley dakika ya 93 Uwanja wa St. James' Park.
  Chelsea imelazimishwa sare ya 2-2 na Watford mabao yake yote yakifungwa na Diego Da Silva Costa dakika ya 32 na 65, wakati ya wageni yamefungwa na Troy Deeney kwa penalti dakika ya 42 na Odion Ighalo dakika ya 56 Uwanja wa Stamford Bridge.
  Bournemouth imelazimishwa sare ya 0-0 na  Crystal Palace Uwanja wa Vitality, wakati bao pekee la Sung-yueng Ki dakika ya tisa Uwanja wa Liberty limeipa Swansea City ushindi wa 1-0 dhidi ya West Bromwich Albion.
  Tottenham Hotspur imeitandika 3-0 Norwich City mabao ya Harry Kane kwa penalti dakika ya 26, dakika ya 42 na Tom Carroll dakika ya 80 Uwanja wa White Hart Lane, wakati Manchester City imeichapa 4-1 Sunderland, mabao yake yakifungwa na Raheem Sterling dakika ya 12, Yaya Toure dakika ya 17, Wilfried Bony dakika ya 22 na Kevin De Bruyne dakika ya 54, wakati la wageni limefungwa na Fabio Borini dakika ya 59 Uwanja wa Etihad.
  Kiungo Mspanyola, David Silva akishangilia na mchezaji mwenzake, Raheem Sterling jana Uwanja wa Etihad PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Aston Villa imelazimishwa sare ya 1-1 na West Ham United, bao lake likifungwa na Jordan Ayew kwa penalti dakika ya 62 na Aaron Cresswell dakika ya 47 Uwanja wa Villa Park, wakati bao pekee la Christian Benteke dakika ya 63 limeipa 
  Liverpool ushindi wa 1-0 Leicester City Uwanja wa Anfield.
  Stoke City jana ilizidi kumuweka pagumu kocha Mholanzi, Louis Van Gaal baada ya kuichapa Manchester United 2-0, mabao ya Bojan Krkic dakika ya 19 na Marko Arnautovic dakika ya 26 Uwanja wa Britannia.
  Christian Benteke (kushoto) akikimbia kushangilia baafa ya kuifungia timu yake bao pekee dhidi ya Leicester jana PICHA ZAIDI GONGA HAPA
  Arnautovic (kushoto) akifumua shuti mbele ya Depay  PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Kwa matokeo hayo, Leicester City inaendelea kuongoza Ligi Kuu England kwa pointi zake 38 baada ya kucheza mechi 18, ikifuatiwa na Arsenal pointi 36 za mechi 18, Manchester City poimti 35 za mechi 18 na Tottenham Hotsput pointi 32 za mechi 18 pia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ARSENAL YATANDIKWA RISASI NNE, CHELSEA YATOA SARE, LIVERPOOL YAIADABISHA LEICESTER, MAN UTD HADI HURUMA! YACHAPWA TENA 2-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top