• HABARI MPYA

  Ijumaa, Desemba 25, 2015

  ROONEY ASEMA; "WACHEZAJI MAN UNITED TUPO NYUMA YA VAN GAAL"

  WAKATI presha ikizidi kwa kocha Louis van Gaal wa Manchester United, Wayne Rooney amesema kwamba wachezaji bado wanapambana kunusuru kibarua cha mwalimu wao.
  United imecheza mechi sita zilizopita katika mashindano yote bila ushindi, ikiwemo kutolewa katika Ligi ya Mabingwa Ulaya kwenye hatua ya makundi na kutupwa nje ya timu nne za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England, huku Mholanzi huyo akitupiwa lawama kwa staili yake ya uchezaji.
  Mtu mzima huyo wa umri wa miaka 69 alikatisha Mkutano na Waandishi wa Habari Jumatano baada ya kuulizwa juu ya kufukuzwa na aliyekuwa kocha wa Chelsea, Jose Mourinho kuwa mbioni kuchukua nafasi yake, lakini Rooney amesema wachezaji bado wapo nyuma ya Van Gaal.

  Wayne Rooney amesema kwamba wachezaji wa Manchester United bado wanapambana kunusuru ajira ya kocha Louis van Gaal PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Akizungumza na Sky Sports, Nahodha huyo wa Manchester United amesema: "Katika wiki chache zilizopita matokeo hayajawa mazuri kwa upande wetu na inatuchanganya kama wachezaji kukabiliana nayo hiyo hali. Lazima tujikaze na kuendelea kushikamana kupigania matokeo tunayoyataka,".
  "Wazi kuna watu kibao wanazungumzia mambo wanayoyaamini yanatokea, wakati kiuhalisi watu wanaandika kwamba benchi la ufundi linajua haswa kinachotokea. Tunajibidiisha, tunampigania kocha kujaribu kugeuza matokeo. Ni muhimu wote bado tumeshikamana,"amesema Rooney.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ROONEY ASEMA; "WACHEZAJI MAN UNITED TUPO NYUMA YA VAN GAAL" Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top