• HABARI MPYA

  Monday, December 28, 2015

  SIMBA SC YAPANGWA NA URA KOMBE LA MAPINDUZI, YANGA YAWEKWA NA AZAM

  Mabingwa watetezi, Simba SC wamepangwa Kundi A pamoja na URA, Jamhuri na JKU
  Na Ali Bakari, ZANZIBAR
  MABINGWA watetezi, Simba SC wamepangwa Kundi A katika Kombe la Mapinduzi 2016 pamoja na URA ya Uganda, Jamhuri ya Pemba na JKU ya Unguja.
  Katika ratiba iliyotolewa leo na Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), mabingwa wa Bara, Yanga SC wamepangwa kundi moja, B pamoja na mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, Mtibwa Sugar ya Morogoro na Mafunzo ya Zanzibar.
  Simba SC itafungua dimba na Jamhuri Januari 2, 2016 mchezo ambao utatanguliwa na mechi kati ya JKU na URA Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
  Yanga SC watashuka dimbani siku inayofuata, Januari 3, 2016 kumenyana na Mafunzo, mchezo ambao utatanguliwa na mechi kati ya Mtibwa Sugar na Azam FC.
  Nusu Fainali zinatarajiwa kuchezwa Januari 9, wakati Fainali itachezwa Januari 13, Uwanja wa Amaan katika kilele cha sherehe za Mapinduzi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAPANGWA NA URA KOMBE LA MAPINDUZI, YANGA YAWEKWA NA AZAM Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top