• HABARI MPYA

  Jumatatu, Desemba 21, 2015

  DIDIER DROGBA KOCHA MSAIDIZI CHELSEA, KILA KITU SAFI NI YEYE TU!

  KOCH wa muda wa Chelsea, Guus Hiddink amethibiths akumtaka gwiji wa klabu hiyo, Didier Drogba awe kocha wake Msaidizi namba moja.
  Hiddink amesema majadiliano yanaendelea kwa sasa na mshambuliaji huyo wa zamani wa Chelsea juu ya namna ya kuuvunja Mkataba wake na timu ya Montreal inayocheza Ligi Kuu ya Marekani (MLS) arejee Stamford Bridge.
  Drogba, ambaye amebakiza mwaka mmoja katika Mkataba wake nchini Canada, aliketi pamoja na babu huyo Mholanzi wa umri wa miaka 69 na mmiliki wa klabu, Roman Abramovich Jumamosi Chelsea ikiifunga Sunderland 3-1.

  Gwiji wa Chelsea, Didier Drogba anatakiwa na Guus Hiddink kurejea Stamford Bridge kama kocha Msaidizi PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Na Hiddink akaliambia gazeti la Telegraaf la Uholanzi kwamba: "Nataka Didier Drogba awe msaidizi wangu. 'Ni muhimu kuwa na magwiji wa klabu kufanya nao kazi. Tatizo pekee, ana Mkataba na Montreal," amesema.’
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: DIDIER DROGBA KOCHA MSAIDIZI CHELSEA, KILA KITU SAFI NI YEYE TU! Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top