• HABARI MPYA

  Thursday, December 31, 2015

  POWER DYNAMOS YAKOPESHWA KINDA MWENYE KIPAJI CHA HATARI ZAMBIA

  KLABU ya Power Dynamos imemsajili mshambuliaji anayeichupukia vizuri, Conlyde Luchanga (pichani kushoto) kutoka Lusaka Dynamos.
  Timu hiyo ya Kitwe imefanya usajili huo wa kushitukiza kwa mchezaji huyo ambaye alikuwa anawaniwa pia na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Faz, Zesco United ambao waliripotiwa kuwa kwenye nafasi nzuri ya kumnasa kinda huyo.
  “Tumekamilisha majadiliano na Lusaka Dynamos kwa ajili ya huduma ya Conlyde," amesema Katibu wa Power Dynamos, Ricky Mamfunda.
  “Amejiunga nasi kwa mkopo kwa Mkataba wa miaka miwili na nusu na tuna fumefurahia sana mapokezi tuliyopewa na Lusaka Dynamos wakati wa majadiliano.”
  Luchanga anawasili Power kuziba pengo la wakali wawili, Alex Ngonga na Jimmy Ndhlovu walioondoka.
  Ngonga aliondoka Juni kwenda kujiunga na CS Mounana ya Gabon wakati Ndhlovu amerejea klabu yake Nkana tangu Julai baada ya kuwa kwa mkopo Power.
  Kuondoka kwa washambuliaji hao kulipunguza makali ya Power katika mbio za taji na kumaliza nafasi ya tatu wakivuna pointi 57 nyuma ya Zanaco walioshika nafasi ya pili kwa pointi zao 63 na Zesco waliokuwa mabingwa kwa pointi zao 67. 
  Wakati huo huo, Lucanga amewasili Uwanja wa Arthur Davies kwa matarajio makubwa baada ya mwanzo mzuri katika Ligi Kuu ya Faz akishinda ya Mchezaji Bora Chipukizi wa Mwaka 2015.
  Luchanga, aliyejiunga na Lusaka Dynamos kutoka klabu ndogo ya Mazabuka United mwanzoni mwa mwaka 2015, amefunga mabao tisa mwaka huu katika klabu yake na mengine mawili kwa timu ya taifa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: POWER DYNAMOS YAKOPESHWA KINDA MWENYE KIPAJI CHA HATARI ZAMBIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top