• HABARI MPYA

  Jumamosi, Desemba 19, 2015

  HOFU YA KUTIMULIWA YAHAMIA KWA VAN GAAL MAN UNITED, ASEMA; "NITAIWEKA WAPI SURA YANGU"

  KOCHA Louis van Gaal anahofia anaweza kuwa kocha afuateye kufukuzwa iwapo Manchester United itapata matokeo mabaa.
  "Sitaki kuondoka hapa kwa kufukuzwa"amesema jana baada ya kushitushwa na habari za kufukuzwa kwa kocha wa Chelsea, Jose Mourinho.
  Lakiniwa chini ya shinikizo Old Trafford iwapo United itacheza japo mechi tano bila ushindi, Van Gaalm amesema anahitaji kuipa matokeo mazuri klabu.
  Mholanzi huyo anaamini bado anaungwa mkono na bodi ya klabu kufuatia kufungwa na Wolfsburg katika Ligi ya Mabingwa Ulaya na Bournemouth katika Ligi Kuu ya England, lakini anapaswa kusginda mchezo wa leo dhidi ya Norwich.

  Kocha wa Manchester United, Louis van Gaal anahofia kumfuata Jose Mourinho aliyefukuzwa Chelsea

  "Najihisi ninajiamini kwa kiasi kikubwa mbele ya bodi na wachezaji wangu,"amesema Van Gaal. "Lakini tunapaswa kupata matokeo, tunafahamu kwamba — wachezaji wanafahamu hili, nafahamu hili binafsi pia na wasaidizi wangu. Tunapaswa kushinda kwa sababu unapofungwa kupita kiasi itakuwa mwisho wa dunia kwangu pia,".
  "Sitaki kuondoka hapa kwa klabu kunifukuza. Hilo litakuwa pigo kubwa mno kusema kwaheri kwa ulimwengu wa soka baada ya kufukuzwa,".
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: HOFU YA KUTIMULIWA YAHAMIA KWA VAN GAAL MAN UNITED, ASEMA; "NITAIWEKA WAPI SURA YANGU" Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top