• HABARI MPYA

  Jumatatu, Desemba 28, 2015

  MESSI ASHINDA TUZO YA MWANASOKA BORA WA MWAKA, BARCA NAYO YANG'ARA

  WASHINDI WA TUZO ZA GLOBE DUBAI 2015 


  Mchezaji Bora wa Mwaka 2015 - Lionel Messi
  Klabu Bora 2015 - Barcelona
  Rais Bora 2015 - Josep Maria Bartomeu
  Mvuto kwenye Vyombo vya Habari - Barcelona
  Tuzo ya Mchezaji Mkongwe- Frank Lampard
  Tuzo ya Mchezaji Mkongwe - Andrea Pirlo
  Wakala Bora 2015  - Jorge Mendes
  Kocha Bora 2015 -  Marc Wilmots
  Akademi Bora 2015 - Benfica
  Mchezaji Bora wa GCC 2015 - Yasir Al-Shahrani
  Refa Bora 2015 - Ravshan Irmatov 
  Lionel Messi (kushoto) akipokea tuzo ya Globe Soccer ya Mchezaji Bora wa Mwaka PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  NYOTA wa Barcelona, Lionel Messi ameng'ara katika usiku wa tuzo za Globe Soccer mjini Dubai baada ya kushinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka.
  Wababe wa La Liga, ambao walishinda mataji matatu msimu uliopita, wameshinda tuzo ya Klabu Bora ya Mwaka, wakati Josep Maria Bartomeu ameshinda tuzo ya Rais Bora wa Mwaka.
  Mshambuliaji huyo wa Argentina, ambaye msimu huu amekuwa benchi kwa muda mrefu kutokakana na majeruhi, amefunga mabao 58 Barca na kufurahia ushindi wa kihistoria wa mataji matatu msimu uliopita.
  "Ni vizuri sana kupokea hizo tuzo, lakini wakati wote nasema timu inafanya haya mambo yawezekane,"amesema Messi. 
  Barcelona, ambayio pia imepewa tuzo ya Mvuto wa Kisoka kwenye Vyombo vya Habari, imeshinda mataji matano mwaka 2015, Ligi ya Hispania, Kombe lka Mfalme, Ligi ya Mabingwa, Super Cup ya Ulaya na Kombe la Dunia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MESSI ASHINDA TUZO YA MWANASOKA BORA WA MWAKA, BARCA NAYO YANG'ARA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top