• HABARI MPYA

  Alhamisi, Desemba 17, 2015

  MOURINHO AFUKUZWA KAZI CHELSEA, HIDDINK KUCHUKUA NAFASI YAKE MARA MOJA

  KOCHA Mreno, Jose Mourinho amefukuzwa kazi Chelsea leo kwa mujibu wa shirika la Utangazaji Uingereza BBC.
  Hiyo inafuatia mabingwa hao wa England, Chelsea kufungwa mechi tisa kati ya 16 za mwanzoni mwa msimu huu, wakiambulia pointi 15.
  Mreno huyo alirejea Stamford Bridge mwaka 2013 na msimu uliopita akaiwezesha timu hiyo kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu na Kombe la Ligi. 
  Kocha Mreno, Jose Mourinho amefukuzwa kazi Chelsea kutokana na matokeo mabaya

  KLABU ALIZOFUNDISHA MOURINHO NA MATAJI ALIYOSHINDA

  Benfica (2000)
  Uniao de Leiria (2001-02)
  Porto (2002-04) mataji mawili ya Ligi, kikombe kimoja na Ligi ya Mabingwa Ulaya moja
  Chelsea (2004-07) mataji mawili ya Ligi Kuu England, moja la FA, mawili ya Kombe la Ligi
  Inter (2008-10) mataji mawili ya Serie A, moja la Coppa Italia, moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya
  Real Madrid (2010-13) taji moja la La Liga, moja la Copa del Rey
  Chelsea (2013-15) taji moja la Ligi Kuu England na moja la Kombe la Ligi
  Taarifa imethibitisha kwamba wameachana na Special One ingawa wamesema matokeo hayakuwa mazuri kiasi cha kutosha.
  "Klabu ya soka ya Chelsea na Jose Mourinho leo wametengana maridhaino na heshima," imesema taarifa hiyo na hatua hiyo inakuja baada ya Chelsea kufungwa mabao 2-1 na Leicester katika Ligi Kuu ya England.
  Guus Hiddink aliyeiongoza timu hiyo kwa muda mwaka 2009, anatarajiwa tena kuchukua nafasi ya Mourinho kwa muda kumalizia msimu na anaweza kuwepo kuiongoza timu katika mchezo dhidi ya Sunderland mwishoni mwa wiki hii.
  Lakini pia Juande Ramos, Brendan Rodgers na Fabio Capello wote wanatakwa katika orodha ya wanaotarajiwa kurithi mikoba ya Mourinho kwa sasa, ingawa mpango wa muda mrefu ni klabu hiyo kumchukua Diego Simeone, ambaye atawagharimu Pauni Milioni 15 kuvunja Mkataba wake na Atletico Madrid. 
  Hii inakuwa mara ya pili Mourinho anafukuzwa Stamford Bridge kwa matokeo mabaya, baada ya awali kufukuzwa katika awamu yake ya kwanza ya kufundisha timu hiyo, mwaka 2007.
  Mmiliki wa Chelsea, bilionea Mrusi Roman Abramovich atalazimika kumlipa Mourinho zaidi ya Pauni Milioni 40 baada ya Mreno huyo kusaini Mkataba wa miaka minne msimu huu.  
  Kocha aliyefukuzwa, Mourinho akiwa na binti yake katika ukumbi wa The Royal Opera House mapema mwaka huu 

  TAARIFA KAMILI YA CHELSEA KUMFUKUZA MOURINHO 

  Klabu ya soka ya Chelsea na Jose Mourinho leo wameachana kwa maridhaino na heshima.
  Wote katika Chelsea tunamshukuru Jose kwa mchango wake mkubwa tangu amejiunga nasi tena mwaka 2013.
  Mataji yake matatu ya Ligi, Kombe la FA, Ngao ya Jamii na matatu ya Kombe la Ligi aliyoshinda katika awamu zake mbili za yanamfanya awe kocha mwenye mafanikio zaidi katika miaka 110 ya historia yetu. 
  Lakini wote, Jose na bodi wamekubaliana matokeo hayakuwa mazuri kiasi cha kutosha msimu huu na kuamini ni vyema pande zote kuachana.
  Klabu inapenda kuweka wazi, Jose anatuacha kwa vipengele vizuri na daima atabakia kipenzi kikubwa, wa kuheshimiwa na mtu muhimu kwa Chelsea. 
  Heshima yake Stamford Bridge na England hakika itamudu na wakati wote anakaribishwa tena Stamford Bridge. Mtazamo wa klabu kwa sasa ni kuhakikisha kikosi chetu chenye vipaji kinakuwa na uwezo.
  Hakutakuwa na maelezo zaidi hadi hapo, uteuzi mpya utakapofanywa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MOURINHO AFUKUZWA KAZI CHELSEA, HIDDINK KUCHUKUA NAFASI YAKE MARA MOJA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top