• HABARI MPYA

  Alhamisi, Desemba 17, 2015

  LIVERPOOL YATAKA KUNG'OA BONGE LA BEKI SCHALKE ILI KUIMARISHA UKUTA WAKE

  KLABU ya Liverpool imeweka wazi dhamira yake ya kumsajili beki wa Schalke, Joel Matip na iko tayari kujadili makubaliano ya Mkataba wa awali na mlinzi huyo mkakamavu.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 alikuwa anatakiwa pia na Newcastle msimu uliopita, lakini Schalke ilitaka dau la Pauni Milioni 10 kwa ajili ya nyota huyo wa Cameroon.
  Liverpool haitaki kutumia fedha nyingi Januari, lakini itaendelea kufuatilia wachezaji maalum kwa maandalizi ya msimu ujao.
  Liverpool imeweka wazi dhamira yake ya kumsajili beki wa Schalke, Joel Matip (kushoto) PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Matip mwenye urefu wa futi 6 na inchi 4, anaweza pia kucheza kama kiungo wa ulinzi na Mkataba wake wa sasa Ujerumani unamalizika mwishoni mwa msimu, hivyo yuko huru kufanya mazungumzo na klabu za nje kuanzia mwezi ujao.
  Timu hiyo ya Anfield pia inaendelea kumfuatilia mchezaji mwenzake Matip, Leroy Sane baada ya mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani kuzuiwa kuondoka msimu uliopita.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YATAKA KUNG'OA BONGE LA BEKI SCHALKE ILI KUIMARISHA UKUTA WAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top