• HABARI MPYA

    Monday, December 21, 2015

    BLATTER NA PLATINI 'WASTAAFISHWA SOKA' KWA KASHFA YA RUSHWA FIFA

    ALIYEKUWA Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Rais Sepp Blatter na Mwenyekiti wa Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA), Michel Platini wamefungiwa kwa miaka nane kutojihusisha na mchezo huo.
    Hatua hiyo inafuatia wawili hao kupatikana na hatia ya ukiukaji maadili, ikiwemo kashfa ya dola za Kimarekani Milioni 2, malipo yasiyo rasmi ambazo alikabidhiwa Patini mwaka 2011, ingawa wameendelea kukana tuhuma hizo.
    Blatter, Rais wa FIFA tangu mwaka 1998, akiwa na umri wa miaka 79, tayari ametangaza kutogombea tena katika uchaguzi wa Februari mwakani.
    Blatter na Platini kulia wote wamezuiwa kujihusisha na soka kwa miaka nane

    Kwa upande wake, Nahodha wa zamani wa Ufaransa, Platini, mwenye umri wa miaka 60 aliyekuwa na nia ya kumrithi Blatter, sasa mpango huo unakufa kifo cha kawaida.
    Platini, mshindi wa mataji matatu ya Ulaya na Mchezaji Bora wa zamani wa Ulaya, amekuwa Rais wa UEFA tangu mwaka 2007. Wawilin wote wamedhamiria kukata rufaa.
    Blatter amesema kuwa atakwenda katika mahakama ya maswala ya michezo (Court of Arbitration for Sport) iliyoko Lausanne kukata rufaa.
    Blatter anasema kuwa malipo hayo yalikuwa ya kazi aliyomfanyia lakini kamati ya uadilifu na nidhamu ya FIFA imewapata na hatia ya kuwa yalikuwa malipo ya kiinua mgongo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BLATTER NA PLATINI 'WASTAAFISHWA SOKA' KWA KASHFA YA RUSHWA FIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top