• HABARI MPYA

  Ijumaa, Desemba 25, 2015

  KOCHA ALIYEIPA U-17 YA NGERIA KOMBE LA DUNIA 'ABWAGA MANYANGA'

  KOCHA wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Nigeria, Emmanuel Amuneke (pichani kushoto) amesema hajisikii tena kuendelea kufundisha Golden Eaglets.
  Amuneke ambaye aliiwezesha Eaglets kutwaa Kombe la Dunia la FIFA kwa vijana chini ya umri wa 17 mwaka 2015 nchini Chile, lakini anaamini amefanya kiasi cha kutosha na sasa anahitaji changamoto mpya.
  Amesema kwamba hana uhakika atakabidhiwa changamoto gani mpya, lakini haitajkuwa na 17 ya Nigeria tena.
  "Nimekuwa kwenye kipengele hiki kwa miaka sasa na kwa kuwa wazi sijisikii tena kuendelea na vijana chini ya umri wa miaka 17. Lazima tuwa wakweli na nafasi zetu. Mmoja anapaswa kusonga mbele na ninaangalia mbele kwenhye changamoto nyingine,"amesema.
  "Tutaona kitakachokuja mbele,” amesema Amuneke ambaye alimrithi Manu Garba ukocha Mkuu wa U-17 ya Nigeria mwaka 2013, akizungumza na Redio Info FM ya Nigeria.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KOCHA ALIYEIPA U-17 YA NGERIA KOMBE LA DUNIA 'ABWAGA MANYANGA' Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top