• HABARI MPYA

  Ijumaa, Desemba 25, 2015

  YANGA SC NA AZAM FC NI PATASHIKA MBIO ZA UBINGWA LIGI KUU, KIVUMBI KUENDELEA KESHO

  RATIBA LIGI KUU YA VODACOM TZ BARA
  Desemba 26, 2015
  Ndanda FC vs JKT Ruvu
  Yanga SC vs Mbeya City
  Majimaji vs Prisons
  Mwadui FC vs Simba SC
  Mtibwa Sugar vs Mgambo JKT
  Coastal Union vs Stand United
  Desemba 27, 2015
  Azam FC vs Kagera Sugar
  Toto Africans vs African Sports
  Desemba 30, 2015
  Azam FC vs Mtibwa Sugar
  Januari 1, 2015
  Ndanda FC vs Simba SC
  Washambuliaji Warundi; Didier Kavumbangu wa Azam FC (kulia) na Amissi Tambwe wa Yanga SC (kushoto) wikiendi hii wanatarajiwa kuzisaidia timu zao katika mbio za ubingwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  YANGA SC inaongoza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, lakini sawa na tajiri mwenye madeni zaidi ya mtaji.
  Kwani, mabingwa hao watetezi wana pointi 30 baada ya kucheza mechi 12, wakati Azam FC iliyocheza mechi 11 ina pointi 29.
  Na Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inaendelea wikiendi hii – kesho Yanga SC wakiwa wenyeji wa Mbeya City Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati keshokutwa Azam FC watakuwa wenyeji wa Kagera Sugar Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Yanga SC itapigania ushindi kesho dhidi ya timu ngumu kutoka Nyanda za Juu Kusini, huku keshokutwa ikiwa na kibarua cha kuiombea duwa njema Kagera Sugar walau ipate sare Chamazi, ili iweke uwiano sawa na Azam FC katika mbio za ubingwa.
  Azam FC nao kesho watakuwa nyuma ya Mbeya City ipate japo sare kwa Yanga SC, ili waendelee kuwa na uwiano mzuri zaidi ya mabingwa hao watetezi katika mbio za ubingwa.
  Simba SC watakuwa wageni wa Mwadui FC kesho Shinyanga

  Kwa ujumla Ligi Kuu inaendelea wikiendi hii, mbali na Yanga SC na Mbeya City – kesho pia Ndanda FC wataikaribisha JKT Ruvu Uwanja wa Nangwanda Sijaon, Mtwara, Majimaji na Prisons Uwanja wa Majimaji mjini Songea, Mwadui FC na Simba SC Uwanja wa Kambarage, Shinyanga, Mtibwa Sugar na Mgambo JKT Uwanja wa Manungu, Turiani Morogoro na Coastal Union na Stand United Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
  Kesho mbali na Azam FC kuikaribisha Kagera Sugar, kutakuwa mchezo mwingine kati ya Toto Africans na African Sports Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza, 
  Azam FC itashuka tena Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Desemba 30 kumenyana na Mtibwa Sugar katika mchezo wake wa kiporo, wakati Simba SC ‘mwaka mpya’ Januari 1, mwaka 2016 watakuwa wageni wa Ndanda FC mjini Mtwara.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA SC NA AZAM FC NI PATASHIKA MBIO ZA UBINGWA LIGI KUU, KIVUMBI KUENDELEA KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top