• HABARI MPYA

  Jumapili, Desemba 20, 2015

  AZAM FC YAITANDIKA MAJIMAJI 2-1, MBEYA CITY ‘ULIMI NJE’ KWA MGAMBO SOKOINE

  RATIBA LIGI KUU YA VODACOM TZ BARA
  Leo; Desemba 20, 2015
  Majimaji 1-2 Azam FC
  JKT Ruvu 2-2 Coastal Union
  Mbeya City 1-1 Mgambo JKT
  Jana; Desemba 19, 2015
  Yanga SC 4-0 Stand United
  Mwadui FC 2-1 Ndanda FC
  Kagera Sugar 1-0 African Sports
  Prisons 0-0 Mtibwa Sugar
  Toto Africans 1-1 Simba SC
  MECHI ZIJAZO…
  Desemba 23, 2015
  Azam FC vs Mtibwa Sugar
  Desemba 26, 2015
  Ndanda FC vs JKT Ruvu
  Yanga SC vs Mbeya City
  Majimaji vs Prisons
  Mwadui FC vs Simba SC
  Mtibwa Sugar vs Mgambo JKT
  Coastal Union vs Stand United
  Desemba 27, 2015
  Azam FC vs Kagera Sugar
  Toto Africans vs African Sports
  Didier Kavumbangu ameifungia Azam FC leo ikishinda 2-1 ugenini

  AZAM FC imepata ushindi muhimu wa ugenini, baada ya kuifunga mabao 2-1 Majimaji Uwanja wa Majimaji Songea jioni ya leo katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Ushindi huo unaifanya Azam FC ifikishe pointi 29 baada ya kucheza mechi 11 na kuendelea kubaki nafasi ya pili, nyuma ya mabingwa watetezi, Yanga SC wenye pointi 30 na mechi moja zaidi.  
  Mshambuliaji wa zamani wa Yanga SC, Didier Kavumbangu alianza kuifungia Azam FC dakika ya 10, kabla ya Ame Ally ‘Zungu’ kufunga la pili dakika ya 20.
  Bao pekee la wenyeji, Majimaji lilifungwa na Alex Kondo dakika ya 55.
  Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Aishi Manula, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Serge Wawa, David Mwantika, Farid Mussa, Frank Domayo, Jean Mugiraneza, Ame Ally/Allan Wanga dk85, John Bocco na Didier Kavumbagu.
  Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, JKT Ruvu imelazimishwa sare ya 2-2 na Coastal Union Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, wakati Mbeya City nayo imelazimishwa sare ya 1-1 na Mgambo JKT Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AZAM FC YAITANDIKA MAJIMAJI 2-1, MBEYA CITY ‘ULIMI NJE’ KWA MGAMBO SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top