• HABARI MPYA

  Jumamosi, Desemba 19, 2015

  YANGA SC YAICHAPA STAND 4-0, TAMBWE APIGA HAT TRICK, SIMBA SC YAKWAMA KWA TOTO

  RATIBA LIGI KUU YA VODACOM TZ BARA
  Leo; Desemba 19, 2015
  Yanga SC 4-0 Stand United
  Mwadui FC 2-1 Ndanda FC
  Kagera Sugar 1-0 African Sports
  Prisons 0-0 Mtibwa Sugar
  Toto Africans 1-1 Simba SC
  Kesho; Desemba 20, 2015
  Majimaji vs Azam FC
  JKT Ruvu vs Coastal Union
  Mbeya City vs Mgambo JKT
  Amissi Tambwe akishangilia baada ya kufunha hat trick leo Yanga ikishinda 4-0

  Na Waandishi Wetu, MWANZA NA DAR ES SALAAM
  YANGA SC imepaa kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kufuatia ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Stand United jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Ushindi huo, unawafanya mabingwa hao watetezi wafikishe pointi 30 baada ya kucheza mechi 12, wakiizidi pointi nne Azam FC ambayo ina mechi mbili mkononi. 
  Shujaa wa Yanga SC leo alikuwa ni Mrundi, Amissi Joselyn Tambwe aliyefunga mabao peke yake, wakati bao lingine limefungwa na Mzimbabwe, Thabani Kamusoko.
  Tambwe alifunga mara tatu mfululizo kipindi cha kwanza, dakika ya 20 akimalizia pasi nzuri ya kiungo Thabani Kamusoko, dakika ya 39 kwa kichwa akimalizia krosi nzuri ya beki wa Juma Abdul na dakika ya 45 akimalizia pasi ya Mzimbabwe Donald Mgoma.
  Katika kipindi hicho, Stand United walipoteza nafasi mbili nzuri za kufunga dakika ya 30 Elias Maguri alipiga nje na dakika ya 44 Haroun Chanongo aligongesha mwamba kipa Deo Munishi ‘Dida’ akiwa amekwishapotea.
  Kamusoko aliifungia Yanga SC bao la nne dakika ya 63 kwa kichwa akiunganisha krosi ya Juma Abdul aliyekuwa katika kiwango kizuri leo.
  Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Deogratius Munish ‘Dida’, Juma Abdul, Mwinyi Hajji, Vincent Bossou, Kelvin Yondani/Pato Ngonyani dk78, Said Juma, Simon Msuva, Thabani Kamusoko, Donald Ngoma/Matheo Anthony dk74, Amissi Tambwe na Deus Kaseke/Godfrey Mwashiuya dk78. 
  Stand United; Frank Muwonge, Nassor Said ‘Chollo’, Abuu Ubwa/Suleiman Mrisho dk78, Revocatus Richard, Philip Metusela, Jacob Massawe, Haroun Chanongo, Amri Kiemba/Jeremiah Katula dk67, Elias Maguri, Suleiman Kassim ‘Selembe’ na Erick Kayombo.
  Mchezo mwingine wa Ligi Kuu leo, Simba SC imelazimishwa sare ya 1-1 na Toto Africans Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
  Simba SC walianza kupata bao dakika ya 22 kupitia kwa Danny Lyanga kabla ya Salmin Hoza kuisawazishia Toto dakika ya 86.
  Mechi nyingine za leo, Mwadui FC imeifunga 2-1 Ndanda FC, Kagera Sugar imeifunga 1-0 African Sports, Prisons imelazimishwa sare ya 0-0 na Mtibwa Sugar.
  Ligi hiyo itaendelea kesho kwa mechi tatu, Majimaji na Azam FC ambayo awali ilikuwa ifanyike leo mjini Songea, JKT Ruvu na Coastal Union na Mbeya City na Mgambo JKT.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA SC YAICHAPA STAND 4-0, TAMBWE APIGA HAT TRICK, SIMBA SC YAKWAMA KWA TOTO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top