• HABARI MPYA

  Jumanne, Desemba 29, 2015

  PETR CHECH SASA NDIYE KIPA MKALI ZAIDI KUWAHI KUTOKEA ENGLAND

  Petr Cech akishangilia jana baada ya kufikisha mechi 170 za Ligi Kuu ya England bila kufungwa PICHA ZAIDI GONGA HAPA


  MAKIPA WALIODAKA MECHI NYINGI BILA KUFUNGWA LIGI KUU ENGKLAND 

  1. Petr Cech                              170 (352)
  2. David James                          169 (572)
  3. Mark Schwarzer                    152 (514)
  4. David Seaman                       142 (344)
  5. Nigel Martyn                           138 (372)
  6. Pepe Reina                            134 (285)
  6. Edwin van der Sar                 134 (314)
  8. Brad Friedel                           132 (450)
  9. Tim Howard                            130 (389)
  10. Peter Schmeichel                 129 (310) 
  KIPA wa Arsenal, Peter Cech ameweka rekodi mpya katika Ligi Kuu ya England, baada ya kufikisha jumla ya mechi 170 za kudaka bila kuruhusu nyavu zake kuguswa.
  Kipa huyo aliyetua Emirates msimu huu akitokea Chelsea, alifikisha rekodi hiyo jana Arsenal ikishinda 2-0 dhidi ya Bournemouth.
  Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 33 hatimaye amevunja rekodi ya kipa wa zamani namba moja wa England, David James - ambaye alikuwa anashikilia rekodi ya kudaka mechi nyingi bila kufungwa kabla ya kustaafu akiwa na Portsmouth mwaka 2010.
  Cech anavunja rekodi hiyo ndani ya jumla ya mechi 352 za Ligi Kuu ya England alizodaka katika klabu za Chelsea na Arsenal.
  James, aliyedaka jumla ya mechi 562, aliweza kuzuia nyavu zake kuguswa katika 169 na kushikilia rekodi ya kipa aliyedaka mechi nyingi za Ligi Kuu ya England bila kufungwa kwa muda mrefu.
  "Ni mafanikio makubwa binafsi na nimejisikia faraja sana mwishoni mwa mchezo ukitazama katika orodha ya makipa waliodaka mechi nyingi bila kufungwa na unaona orodha ya makipa waliokuwa wanacheza na ambao bado wanacheza katika ligi hii, kisha wazi ni mafanikio makubwa kuongoza katika orodha," amesema.
  Kipa huyo wa kimataifa wa Czech, alitua Arsenal baada ya miaka 11 ya kupiga kazi Stamford Bridge.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: PETR CHECH SASA NDIYE KIPA MKALI ZAIDI KUWAHI KUTOKEA ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top