• HABARI MPYA

  Tuesday, December 22, 2015

  VAN GAAL AWAPA MANENO MAZITO WACHEZAJI NA VIONGOZI MAN UNITED, AWAAMBIA; "TUSHIKAMANE"

  KOCHA Louis van Gaal ametoa hotuba yenye hisia kali jana kwa wachezaji Manchester United na viongozi katika jithada za kuokoa kibarua chake akisema wanapaswa kushikamana katika kipindi hiki kigumu.
  Kocha huyo wa United alipigiwa makofi na karibu watu 200 wakati sherehe ya Krisimasi makao makuu ya klabu, viwanja vya Carrington iliyokwenda sambamba na chakula cha mchana.
  "Sisi ni Manchester United na tutakuwepo — lakini lazima tushikamane," huo ndiyo ulikuwa ujumbe wa Van Gaal ingawa utamaduni wa asili wa mechi ya timu za vijana za United uliahirishwa.

  Kocha Louis van Gaal ametoa hotuba yenye hisia kali jana wakati wa sherehe za Krisimasi Manchester United jana mchana PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Van Gaal anakabiliwa na shinikizo baada ya kucheza mechi tatu mfululizo bila ushindi, mara ya mwisho Jumamosi akifungwa 2-1 nyumbani na  Norwich City.
  Wamiliki wa United, Wamarekani familia ya Glazer, na Mwenyekiti, Ed Woodward inafahamika wanafikiria kufanya mabadiliko ya benchi la Ufundi na wamefanya mawasiliano na wawakilishi wa kocha Mreno, Jose Mourinho, ambaye alifukuzwa Chelsea wiki iliyopita. 
  Mourinho tayari ameweka wazi kwamba yuko tayari kurejea kazini haraka.
  Vyanzo vya habari ndani ya United vinasema kwamba klabu hiyo inafanya mpango wa kumshawishi Mourinho kupitia wakala wake, Jorge Mendes ili atue Old Trafford. 
  Mendes ni mtu aliyefanya kazi kwa karibu na kocha Sir Alex Ferguson na Mtendaji Mkuu wa zamani, David Gill aliyewasaidia kuwapata nyota kama Cristiano Ronaldo, Nani, Anderson, Bebe na David de Gea wakatua United.
  Siku za karibuni amekuwa akifanya kazi na Woodward pia na ndiye aliyefanikisha mipango ya kusajiliwa kwa Radamel Falcao na Angel di Maria, pamoja na De Gea kukubali kusaini Mkataba mpya.
  Pamoja na hayo, Van Gaal anataka kutumia fursa hii kurudisha matokeo mazuri ndani ya klabu wakati wa Krisimasi akikabiliwa na mechi ngumu dhidi ya Stoke City na Chelsea.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: VAN GAAL AWAPA MANENO MAZITO WACHEZAJI NA VIONGOZI MAN UNITED, AWAAMBIA; "TUSHIKAMANE" Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top