• HABARI MPYA

  Ijumaa, Desemba 18, 2015

  YANGA SC WALALAMIKIA KUCHEZESHWA LIGI KUU WAKATI SIMBA NA AZAM FC HAWACHEZI

  RATIBA LIGI KUU YA VODACOM TZ BARA
  Leo; Desemba 19, 2015
  Yanga SC vs Stand United
  Mwadui FC vs Ndanda FC
  Kagera Sugar vs African Sports
  Prisons         vs Mtibwa Sugar
  Toto Africans vs Simba SC
  Majimaji         vs Azam FC
  Desemba 20, 2015
  JKT Ruvu vs Coastal Union
  Mbeya City vs Mgambo JKT
  Jerry Muro pia ametumia mkutano huo kutambulisha wachezaji wapya wa Yanga SC, kulia ni Issoufou Boubacar Garba kutoka Niger

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  YANGA SC imelalamikia kuchezeshwa mfululizo mechi za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, wakati wapinzani wao, Azam FC na Simba SC hawachezi.
  Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga SC, Jerry Muro amewaambia Waandishi wa Habari katika Mkutano uliofanyika makao makuu ya klabu Jangwani, Dar es Salaam kwamba hawapendezewi na mwenendo huo.  
  “Tunakwenda kucheza kesho na Stand United, lakini wenzetu bado wana viporo na hawachezi. Hizi ni figisu, ilifaa wote tucheze pamoja.
  Wakiendelea kufanya hivi, tutatumbua majipu,”. “Kwa nini tuachiwe sisi tu tucheze wakati wenzetu wakae watutazame, si jambo zuri. Tuwaombe wenye kusimamia kanuni na sheria za mpira Tanzania waliangalie hili,”amesema Muro.
  Yanga SC inatarajiwa kushuka dimbani kesho kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kumenyana na Stand United ya Shinyanga ukiwa ni mchezo wa tatu ndani ya siku 10, baada ya Jumamosi iliyopita kutoa sare ya 0-0 na Mgambo JKT na Jumatano kushinda 1-0 dhidi ya African Sports Uwanja wa Mkwakwani, Tanga. 
  Wapinzani wa Yanga SC katika mbio za ubingwa, Azam FC walimenyana baina yao Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kutoa sare ya 2-2, lakini katikati ya wiki walikuwa mapumzikoni, ingawa kesho nao watakuwa kazini tena.
  Azam FC watakuwa Uwanja wa Majimaji Songea kumenyana na wenyeji, Majimaji wakati Simba SC watakuwa wageni wa Toto Africans Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza. 
  Jerry Muro pia ametumia Mkutano huo kuwatambulisha wachezaji wapya wa Yanga SC, Paul Nonga kutoka Mwadui FC na Issoufou Boubacar Garba kutoka Niger.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA SC WALALAMIKIA KUCHEZESHWA LIGI KUU WAKATI SIMBA NA AZAM FC HAWACHEZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top