• HABARI MPYA

    Tuesday, December 22, 2015

    ARSENAL YAICHAPA 2-1 MAN CITY NA KUONGEZA KASI MBIO ZA UBINGWA ENGLAND

    TIMU ya Arsenal imeweka hai matumaini ya ubingwa, kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Manchester City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa jana Uwanja wa Emirates.
    Ushindi huo unaifanya Arsenal iendelee kukamata nafasi ya pili kwa kufikisha pointi 36, baada ya kucheza mechi 17, ikizidiwa pointi mbili na vinara Leicester City.
    Manchester City inaendelea kubaki nafasi ya tatu kwa pointi zake 32 za mechi 17, wakati Tottenham Hotspur ni ya nne kwa pionti zake 29 sawa na Manchester United, zote zikiwa zimecheza mechi 17 pia.

    Olivier Giroud akishangilia baada ya kuifungia bao la pii jana PICHA ZAIDI GONGA HAPA

    Mshambuliaji wa England, Theo Walcott alianza kuifungia Arsenal dakika ya 33 Uwanja wa kwa pasi ya kiungo Mjerumani Mesut Ozil aliyemsetia pia mshambuliaji Mfaransa Olivier Giroud kufunga la pili dakika ya 46.
    Sergio Aguero alirejea uwanjani jana baada ya kukosekana muda mrefu kutokana na majeruhi, lakini akacheza kwa dakika 63 tu kabla ya kumpisha Wilfried Bony baada ya kushindwa kufunga.
    Mwanasoka Bora wa Afrika, Yaya Toure ndiye aliyeifungia Manchester City bao la kufutia machozi dakika ya 82.
    Kikosi cha Arsenal kilikuwa; Cech, Bellerin, Mertesacker, Koscielny, Monreal, Ramsey, Flamini, Walcott/Chambers dk88, Ozil/Oxlade-Chamberlain dk76, Campbell/Gibbs dk70 na Giroud.

    Manchester City; Hart, Sagna, Otamendi, Mangala, Kolarov, Fernandinho, Toure, Delph/Sterling dk46, De Bruyne, Silva/Navas dk73 na Aguero/Bony dk63.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ARSENAL YAICHAPA 2-1 MAN CITY NA KUONGEZA KASI MBIO ZA UBINGWA ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top