YANGA SC itacheza na Etoile du Sahel ya Tunisia katika hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho Afrika katikati ya mwezi huu.
Hiyo inafuatia wana Jangwani hao kuvuka vizingiti viwili, kwanza kuitoa BDF ya Botswana na baadaye FC Platinum ya Zimbabwe.
Etoile iliyoanzia Raundi ya Kwanza moja kwa moja, yenyewe imefuzu hatua hii baada ya kuing’oa Benfica de Luanda ya Angola.
Mara tu baada ya kuthibitika, Yanga itacheza na Etoile kumeanza kutokea kauli za kukatisha tamaa, kwamba huo ndiyo mwisho wa safari ya timu ya Tanzania katika michuano ya mwaka huu.
Wanaosema hivyo, wakiwemo Waandishi wa Habari na Wachambuzi wa masuala ya michezo, wanazingatia historia, kwamba Yanga haina utamaduni wa kufurukuta mbele ya timu za Kaskazini mwa Afrika.
Wanazingatia historia- ni kweli kihistoria Yanga haijawahi kuitoa timu ya Kaskazini mwa Afrika katika michuano ya Bara hili.
Lakini pamoja na ukweli huo, mambo yanabadilika na soka yenyewe kwa kiasi kikubwa imebadilika.
Zile zama za lazima Yanga ikikutana na timu ya Kaskazini itafungwa zimekwishapitwa na wakati.
Tumeona mfano mwaka jana katika Ligi ya Mabingwa Afrika, Yanga ilikaribia kuitoa Al Ahly ya Misri- kama si kung’olewa kwa mikwaju ya penalti, baada ya sare ya jumla ya 1-1.
Matokeo yale yalifanya watu wengi waione kama Ahly ya mwaka jana ilikuwa timu dhaifu, lakini mwishowe ikaenda kubeba Kombe la Shirikisho.
Wakati umefika sasa watu waachane na dhana za kizamani, badala yake wauzungumzie mchezo wa soka kiuhalisia wake, tena wakitoa hoja za kitaalamu na tathmini za kina.
Tutazame kikosi cha sasa Yanga SC kina wachezaji wa aina gani- utagundua ni kikosi imara chenye wachezaji wengi waliokaa pamoja kwa muda mrefu na kuzoeana.
Ni kikosi ambacho kina wachezaji wenye uzoefu mkubwa wa michezo ya kimataifa, ambacho kama kitapatiwa maandalizi mazuri ya kisayansi, kinaweza kubadilisha hiyo tunayoiita historia.
Sioni mantiki ya kuanza kuikatisha tamaa Yanga SC mapema, kwa sababu hata Etoile yenyewe inaonekana si timu ya kutisha.
Imefuzu kwa ushindi wa jumla wa 2-1 baada ya kushinda 1-0 nyumbani na kwenda kutoa sare ya 1-1 ugenini, wakati Yanga imeshinda jumla 5-2, ikishinda 5-1 nyumbani na kwenda kufungwa 1-0 ugenini.
Ni hivi karibuni timu yetu ya taifa iliifunga Morocco 3-1 Dar es Salaam katika mchezo wa kufuzu Fainali za Kombe la Dunia na katika mechi ya marudiano wakatufunga 2-1 kwao, tena baada ya hila nyingi.
Hiyo ilikuwa ni katika mechi za makundi, kama zingekuwa mechi za mtoano, ina maana Tanzania ingeitoa Morocco.
Hii inatosha kutufanya tuamini mambo yamebadilika na zile zama za kutabiri kwa kuzingatia historia zimepitwa na wakati- na sasa watu wanaangalia uhalisia.
Yanga SC wanatakiwa wajiandae kwa mechi mbili ngumu, nyumbani na ugenini, lengo likiwa kupata matokeo mazuri na kusonga mbele.
Mapema, naomba niwe sehemu ya Watanzania wachache wanaoamini Yanga inaweza kuitoa Etoile, iwapo itajiandaa vizuri ndani na nje ya Uwanja.

.png)
0 comments:
Post a Comment