Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
ALIYEKUWA Mfadhili Mkuu wa Coastal Union ya Tanga, Nassor Bin Slum amerejea kuokoa jahazi, baada ya timu hiyo kuanza kuyumba.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY leo mjini Dar es Salaam, Bin Slum amesema kwamba amerejea baada ya kuombwa na wanachama wengi wa Coastal ili akaokoe jahazi. Amesema naye akiwa mwanachama wa muda mrefu wa Coastal, hajaridhishwa na mwenendo wa timu kwa sasa, ndiyo maana ameamua kurejea.
“Nimerejea maalum kuisaidia timu ili isishuke daraja, baada ya kuombwa na wana Coastal wenzangu. Nimezungumza na viongozi wanaohusika na timu kwa sasa, na wao wamekubali nirejee kuwasaidia. Kwa hiyo nasubiri majibu yao rasmi, ili niingie kazini,”amesema Bin Slum.
Bin Slum alijtoa Coastal Union mwaka jana, baada ya kuingia kwenye mgogoro na aliyekuwa Mwenyekiti wa klabu, Ally Hemed ‘Aurora’.
Baada ya kujitoa Coastal, Bin Slum akaingia mikataba ya kuzidhamini timu tatu za Ligi Kuu, Stand United, Ndanda FC na Mbeya City.
Aurora naye hakudumu Coastal, kwani alijiuzulu baadaye mwaka jana na timu kuwa chini ya Makamu Mwenyekiti, Stephen Mnguto, ambaye naye kwa bahati mbaya akawa hajishughulishi na masuala ya timu.
Kwa sababu hiyo, timu ikawa chini ya Katibu Mkuu Kassim El Siagi na Meneja Akida Machai, ambao chini yao hali imekuwa tete barabara ya 13.
Nassor Bin Slum kulia akitiliana saini mikataba ya udhamini na Katibu wa Ndanda FC, Edmund Kunyengana kushoto mwaka jana
Coastal Union inashika nafasi ya saba hivi sasa katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ikiwa na pointi 24 za mechi 21 na katika mechi tano ilizobakiza, nne ni za ugenini, tena dhidi ya timu ambazo zipo kwenye hali mbaya, au zinapigania ubingwa.
Tayari kikosi cha Coastal Union kimewasili Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo wa kesho wa Ligi Kuu dhidi ya vinara, Yanga SC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

![]() |
| Nassor Bin Slum amerejea Coastal Union kuokoa jahazi |

.png)
0 comments:
Post a Comment