• HABARI MPYA

    Wednesday, April 08, 2015

    YANGA, HEBU TUONDOLEENI HILI `JINAMIZI` LA KUTESWA NA WAARABU

    Na Hemed Kivuyo, DAR ES SALAAM
    AWALI ya yote niwashukuru wote mliyonitumia ujumbe na kutoa maoni yenu katika Makala mbalimbali Niliyokuwa nikiandika katika `Uga` huu. Haijalishi mlinikosoa, kunipongeza ama vyovyote vile. Nawashukuru.
    Niwape `Kongole` wanayanga kwa kufanikiwa kuwatupa Nje Fc Platnum kwa Jumla ya Mabao 5-2. Ni hatua Nzuri kwa wawakilishi hawa wa Tanzania kufikia hatua hiyo zaidi sana wakiwa wamebeba Bendera ya Taifa la Tanzania.
    Ni Wazi wala huitaji kuwa na elimu ya chuo kikuu kuiona Timu ya Yanga Ndiyo timu Yenye Wachezaji waliyocheza pamoja kwa muda mrefu na inaonekana Ndiyo timu iliyosajili kwa umakini wa hali ya juu ingawa kuna baadhi ya maeneo yanaonekana kuhitaji marekebisho madogo.
    Kabla ya Yanga haijabaki Yenyewe kuiwakilisha Tanzania katika Michuano ya Kimataifa Tuliyoona Azam fc ikiondolewa Katika Michuano Mikubwa Afrika Dhidi ya El –Mereck ya Sudan. El-Mereck hawana Tofauti na Timu za Misri,Saudi Arabia,Tunisia na Ndugu zao.
    Wanacheza Soka Nje ya Soka kwa 50%, wanacheza na waamuzi kwa 20% na wanacheza Soka uwanjani kwa dakika 60 badala ya 90 kutokana na `kupoteza muda kipuuzi` hasa wanapokuwa ugenini.
    Kwa wanaowafuatilia `waarabu` hao watakubaliana nami juu ya `upuuzi` huo wa Waarabu.
    Yanga itaanzia hapa Nyumbani ( Tanzania) kibarua chake Dhidi ya Etohil-Du-Sahil .Binafsi sikufurahishwa na Yanga kuanzia Nyumbani. Nasema hivyo kwasababu `waarabu` watakuja hapa kupooza mpira na kupoteza Muda ili wafungwe idadi ndogo ya Mabao.
    Nyota tegemeo la mabao Yanga SC, Mrisho Ngassa kulia, Simon Msuva katikati na Amisi Tambwe kushoto, je watatikisa nyavu za Waarabu?

    Wakifanikiwa katika lengo lao hilo watakwenda Nyumbani kwao kujipanga.Watajipanga kuanzia nje ya uwanja,kwa maana ya kuanzia uwanja wa Ndege,Hotelini,Kambini,Kwa waamuzi, na kila aina ya hila .
    Kama Yanga imedhamiria kufuta `uteja` kwa Timu zenye asili ya kiarabu basi ni lazima Yanga ishinde zaidi ya mabao mawili au matatu kwa sufur na baada ya hapo wajipange sawasawa watakapokwenda Tunisia. Wajipange kuanzia Uwanja wa Ndege,Hotelini na namna ya kukabiliana na Waamuzi ambao ni wazi `watawanyonga` Yanga ( hili lipo wazi kabisa,na huitaji kuwa na elimu ya chuo kikuu kulitambua)
    Ikifanikiwa hilo Yanga itakuwa Imetuondoa katika `uteja` Dhidi ya waarabu. Itakuwa imeshinda mara tatu,kwa maana itakuwa imeshinda dhuluma,imeshinda maamuzi batili ya waamuzi,imeshinda zengwe nje ya uwanja na imeshinda katika soka ndani ya uwanja.
    Wachezaji na viongozi wa Yanga watambue kuwa ,wanakuja kucheza na Timu yenye `hila` Nyingi kuanzia Nje ya uwanja mpaka Ndani.
    VIONGOZI:
    Uwendawazimu ni hali mtu kurudia jambo lile lile wakati uleule akitaraji majibu tofauti. Ni lazima tujifunze kutokana na makosa. Mimi Ni mmoja kati ya watu wanaoamini kuwa Yanga ina viongozi makini sana.
    Hata TFF nao wanahusika katika somo hili. Watakuja hapa Etohil du sahil, kama kuna ulazima wakwenda kuwapokea tuwaache uwanja wa Ndege kwa zaidi ya saa tano, kama kuna ulazima wa kuwapa gari basi tuwape gari bovu lenye kutoa moshi ndani, kama kuna ulazima wakuwatafutia Hoteli tuwape Hoteli isiyokuwa na hadhi.
    Kikosi cha Etoile du Sahel
    Kikosi cha Yanga SC

    Siku moja kabla ya Pambano watafanya mazoezi uwanja wa Taifa,kama watahitaji kuanzia saa kumi basi tuwape uwanja kuanzia saa kumi nambili kasoro. Wazuiwe mlangoni,wapewe sababu dhaifu za kutokupewa uwanja kwa muda huo kama wao watakavyotoa sababu dhaifu huko kwao.Tuwatolee maneno makali yasovikwa `nguo.
    Nayasema haya bila kutania hata kidogo. Tutakuwa tunafanya `uwendawazimu` kurudia makosa kila mwaka. Naamini kufanya hivyo siyo kosa kwakuwa kama ni kosa tungeona El Mereck,Zamaleck,etohil zikichukuliwa hatua miaka yote wanavyofanya hivyo. Ni `kiherehere` chetu kuwafanyia uungwana usokuwa na faida miaka yote.
    Tukiyafanya hayo tutakuwa tumeshapata ushindi kwa 50%. Nahata tusipoyafanya hayo `kwa ujinga` wetu wao watafanya hivyo tu ( mwenye kubisha ahifadhi haya maandishi) na nikwanini tusifanye kwakuwa siyo kosa!!!!!! Hebu tuuvae uwendawazimu. Kule kwao ni lazima vitu hivi vifanyike.
    POLISI.
    Polisi waache `kiherehere` kama wao ni wazalendo zaidi basi waende Tunisia kuzuia machafuko na siyo kuwakingia kifua `waarabu` kwakuwasindikiza na kuwapa pikipiki majiani, Muwende kuwachukua hotelini saa tisa na dakika 15, ikibidi musiende kabisa kuwachukua .( waje wenyewe na balozi wao)
    Muawache mara moja kuwatisha watanzania watakokuwa na bendera ya Taifa la Tanzania na watakaa popote Jukwaani. Siyo kwenda kuwafukuza mashabiki `watanzania` eneo ambalo hukaa mashabiki mashabiki wachache wa Etohil. Ni kiherehere ambacho Polisi wa Nchi yeyote hawana zaidi ya Tanzania. Polis wanapaswa kuongoza kwa Uzalendo na Nchi yao.nayasema haya kwasababu nimeshaona kwa Nchi za wenzetu hasa huko kwa `Waarabu`.

    WACHEZAJI YANGA
    Wafahamu katika mchezo huo utakaokuwa wa dakika 90,wao `waarabu` watalazimisha kucheza kwa dakika 70 au 60. Watajiangusha bila sababu za msingi,watacheza taratibu,watakuwa walalamishi kwa mwamuzi ili kuomba huruma ya mwamuzi. Watajiangusha eneo la 18 kutafuta Penalti hata kama hawajaangushwa.
    Wanachotakiwa kufanya wachezaji wa Yanga pamoja na kufuata maelekezo Waalimu wao ,ni kucheza kwa kasi bila kuwaiga,ni kutumia nafasi wanazopata ili kupata magoli mengi zaidi.
    Kutoruhusu `waarabu` kuingia eneo la 18 mara kwa mara kwakuwa akili za Mwamuzi hakuna anayejua hata kama atadanganywa anaweza kutoa Penalti. Ukimgusa tu katika eneo hilo ataanguka kama vile kaangukiwa na mfuko wa saruji.
    Wachezaji wa Yanga waache `mzaha` hasa wanapofika katika eneo la 18,watumie nafasi wanazopata ili kupata magaoli.
    Wachezaji wa Yanga wacheze ili kutafuta magoli na siyo kupooza mpira na kukubali mfumo wa wapinzani.
    Washambuliaji wa Yanga wanaotokea Pembeni,kama Msuva pamoja na kuwa na mbio na uwepesi pia atumie akili muda mwingi,sehemu ya kutoa pasi atoe,sehemu ya kupiga apige,amiliki mpira ndani ya 18.Viungo wa Yanga ,salum Telela,Haruna Niyonzima,na kama atakuwepo Said Juma wahakikishe wanatoa pasi za harakaharaka na kuwalisha mipira mawinga wa pembeni ambao nao wanapaswa kutoa `krosi` kama wataona Tambwe tayari yupo ndani ya 18. Asipoona mtu eneo hilo aendelee kumiliki mpira kuelekea ndani ya 18
    Wahakikishe wanatoa pasi za mbali kwa mawinga kwakuwa kuna mawinga wenye mbio.
    Kanavaro,Yondani na Mbuy Twite waache masihara kule Nyuma ,wasiruhusu `waarabu` wamili mipira ndani ya 18. Wasijiamini sana kwakucheza pasi za muda mrefu eneo la Nyuma.
    Wachezaji Yanga wahakikishe mpaka mapumziko wapo mbele kwa mabao mawili au zaidi. Hapo mtawanyima kupoteza muda. kuna mengi lakini naomba niishie hapa. 

    (Mwandishi wa makala haya ni mtangazaji wa ITV na Redio One, anapatikana kwa email medkivuyo11@yahoo.com na nambari za simu +255 752 250157 au +255 655 251057) 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA, HEBU TUONDOLEENI HILI `JINAMIZI` LA KUTESWA NA WAARABU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top