• HABARI MPYA

    Tuesday, April 14, 2015

    RONALDO NA MESSI KUCHEZA TIMU MOJA, NI KATIKA 'GEMU' LA UEFA ALL STAR

    WANASOKA wawili mahasimu, Lionel Messi na Cristiano Ronaldo wanaweza kujikuta katika kikosi kimoja kucheza mechi ya UEFA All-Star itakayohusisha wachezaji bora zaidi Ulaya, kwa mujibu wa taarifa kutoka Hispania.
    Wanaweza kuchezea 'Team South', nyoa wa Ulaya Kusini ambao watatoka katika Ligi za La Liga ya Hispania, Serie A ya Italia na Ligue 1 ya Ufaransa dhidi ya 'Team North', nyota wa Ulaya Kaskazini wanaotoka Ligi Kuu ya England, Bundesliga ya Ujermani na Ligi Kuu ya Urusi.
    Gazeti la Mundo Deportivo limeripoti kwamba kampuni ya Masoko imeiomba UEFA juu ya mchezo huo na kupendekeza ifanyike kila mwaka baada ya kuvutiwa na na mechi ya NBA All-Star baina ya Western na Eastern Conferences (Kanda ya Mashariki na Magharibi).
    Messi and Ronaldo would be the star attractions in the 'North vs South' All-Star fixture
    Messi na Ronaldo wanaweza kuungana katika kikosi kimoja kucheza mechi kati ya 'North dhidi ya South' All-Star

    WANAOTARAJIWA KUWAMO VIKOSI VYA ALL-STAR YA UEFA 

    South: Buffon; Danilo, Sergio Ramos, Pique, Thiago Silva; Messi, Pogba, Koke, Neymar; Cristiano Ronaldo, Ibrahimovic
    North: Neuer; Terry, Hummels, Alaba; Robben, Di Maria, Silva, Reus; Alexis, Aguero, Hazard
    Wachezaji wa kuchezea timu hizo watachaguliwa kwenye mitandao kutokana na kura za mashabiki na klabu moja haitapewa fursa ya kutoa zaidi ya wachezaji watatu.
    Lakini pamoja na ukweli huo, uhondo wa mecbi hiyo utaletwa na nyota wa Barcelona, Messi na Neymar kuungana na mahasimu wao wa Real Madrid, Ronaldo na Gareth Bale.
    Nyota wengine wa Kusini wanaopewa nafasi kubwa ya kuwamo kwenye kikosi cha 'Team South' ni pamoja na mshambuliaji wa Paris Saint-Germain, Zlatan Ibrahimovic na kiungo wa Juventus, Paul Pogba.
    Upande wa 'Team Kaskazini' bila shaka nyota kama washambuliaji wa Manchester City, Sergio Aguero, Man United, Wayne Rooney, winga wa Chelsea, Eden Hazard, winga wa Manchester United, Angel di Maria na kipa wa Bayern Munich, Manuel Neuer wanatarajiwa kuwamo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RONALDO NA MESSI KUCHEZA TIMU MOJA, NI KATIKA 'GEMU' LA UEFA ALL STAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top