![]() |
| Prisons wanashika nafasi ya pili kutoka mkiani |
Mjini Morogoro wakata miwa wa Mtibwa Sugar watakua wenyeji wa maafande wa jeshi la Magereza nchini timu ya Tanzania Prisons kutoka Mbeya, mchezo utakaopigwa katika dimba la Manungu Turiani.
Azam FC inahitaji ushindi kesho ili kufufua matumaini ya kutetea ubingwa wake, baada ya sare mbili mfululizo 1-1 zote, dhidi ya Mtibwa Sugar na Mbeya City, ambazo zimewafanya wazidiwe pointi nane na vinara, Yanga SC (46-38).
Mtibwa Sugar nao wanahitaji ushindi katika mchezo huo, kama ilivyo kwa Prisons ili kujiondoa katika mazingira ya kushuka daraja. Mtibwa ina pointi 24 za mechi 21, ikiwa inashika nafasi ya 11, wakati Prisons yenye pointi 21 za mechi 21, inashika nafasi ya 13 katika ligi ya timu 14.



.png)
0 comments:
Post a Comment