• HABARI MPYA

    Saturday, April 18, 2015

    AZAM FC YAZINDUKA, YAICHAPA 2-1 KAGERA SUGAR, UBINGWA BADO HAUNA MWENYEWE

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    AZAM FC wamezinduka kutoka kwenye sare tatu mfululizo, baada ya jioni ya leo kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
    Mabingwa hao watetezi, Azam FC sasa wanatimiza pointi 42, baada ya kucheza mechi 22, nyuma ya vinara, Yanga SC wenye pointi 46 za mechi 21.
    Azam ilipata bao lake la kwanza dakika ya 43 kupitia kwa kiungo wake, Frank Domayo aliyepiga shuti kali baada ya pasi ya Didier Kavumbagu.

    Kagera Sugar ilipata bao la kusawazisha dakika ya 52, mfungaji Babu Ally Seif aliyetokea benchi kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Paul Maona.
    Winga Mganda, Brian Majwega aliifungia Azam FC bao la pili dakika ya 80 baada ya kuipangua ngome ya Kagera Sugar, ambayo leo iliongozwa na beki wa zamani wa Yanga SC, Ibrahim Job.
    Kikosi cha Azam FC kilikuwa: Aishi Manula, Gardiel Michael, Shomary Kapombe, Aggrey Morris, Serge Wawa, Frank Domayo/Amri Kiemba dk76, Mudathir Yahya/Bryson Raphael dk89, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Brian Majwega, Gaudence Mwaikimba na Didier Kavumbagu. 
    Kagera Sugar: Andrew Ntalla, Malegesi Mwanga, Salum Kanoni, Ibrahim Job, Abubakar Mtiro, George Kavila, Paul Maona/Babu Ally Seif dk46, Atupele Green, Paul Ngwai, Rashid Mandawa/Adam Kingwande dk47 na Victor Hangaya.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC YAZINDUKA, YAICHAPA 2-1 KAGERA SUGAR, UBINGWA BADO HAUNA MWENYEWE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top