• HABARI MPYA

    Saturday, April 18, 2015

    BARCA YAITIMULIA MAVUMBI REAL LA LIGA, MESSI APIGA LA 400

    BARCELONA imeendelea kuitumulia vumbi Real Madrid katika mbio za taji la La Liga, baada ya jioni ya leo kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Valencia Uwanja wa Camp Nou.
    Luis Suarez aliifungia Barcelona dakika ya kwanza, kabla ya Claudio Bravo kupangua penalti Nahodha wa Valencia, Dani Parejo dakika ya tisa. 
    Lionel Messi akaihakikishia Barca pointi tatu dakika ya 90, ambalo linakuwa bao lake 400 tangu aanze kuichezea Barcelona.
    Barca sasa inatimiza pointi 78 baada ya kucheza mechi 32, ikifuatiwa na Real yenye pointi 73 za mechi 31. Real inamenyana na Malaga baadaye usiku huu.
    Lionel Messi (left), Luis Suarez (centre) and Neymar celebrate Suarez's goal in the first minute for Barcelona against Valencia
    Lionel Messi (kushoto), Luis Suarez (katikati) na Neymar wakishangilia bao la Suarez dhidi ya Valencia leo
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BARCA YAITIMULIA MAVUMBI REAL LA LIGA, MESSI APIGA LA 400 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top