• HABARI MPYA

    Saturday, April 04, 2015

    ARSENAL YAIPA KIPIGO ‘CHA PAKA JIZI’ LIVERPOOL

    KLABU ya Arsenal imeifumua mabao 4-1 Liverpool Uwanja wa Emirates jioni ya leo katika mchezo wa Ligi Kuu ya England na sasa ubingwa inawezekana kwa Washika Bunduki wa London.
    Arsenal inapanda hadi nafasi ya pili baada ya kutimiza pointi 63 kutokana na mechi 31, ikizidiwa pointi nne na vinara, Chelsea.
    Hector Bellerin aliifungia Arsenal dakika ya 37, kabla ya Mesut Ozil kufunga la pili dakika tatu baadaye kwa shuti la mpira wa adhabu.
    Alexis Sanchez akafunga bao la tatu dakika ya 45 kabla ya Raheem Sterling kuangushwa na Bellerin na kuwa penalti iliyotiwa nyavuni na Jordan Henderson dakika ya 76 kuipatia Liverpool bao la kufutia machozi.
    Emre Can alitolewa kwa kadi ya nyekundu baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano na kuiachia pengo Liverpool zikiwa zimebaki dakika tano mchezo kumalizika.
    Mchezaji Bora wa Ligi Kuu England mwezi Machi, Olivier Giroud akaifungia Arsenal bao la nne dakika ya mwisho. 
    Kikosi cha Arsenal kilikuwa; Ospina, Bellerin, Mertesacker, Koscielny/Gabriel dk49, Monreal, Coquelin, Cazorla, Ramsey/Flamini dk62, Ozil/Welbeck dk73, Sanchez na Giroud.

    Liverpool; Mignolet, Can, Toure, Sakho, Henderson, Lucas, Allen, Moreno, Markovic/Sturridge dk46, Sterling na Coutinho.
    Alexis Sanchez celebrates with Olivier Giroud after his stunning strike from just outside the penalty area made it 3-0 to Arsenal in the first half
    Alexis Sanchez akishangilia na Olivier Giroud baada ya kuifungia bao la tatu Arsenal katika ushindi wa 4-1 dhidi ya Liverpool 

    PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-3025492/Arsenal-4-1-Liverpool-Hector-Bellerin-Mesut-Ozil-Alexis-Sanchez-strike-half-blitz-Olivier-Giroud-s-clincher-leave-Brendan-Rodgers-four-hopes-tatters.html#ixzz3WLio7CEo 

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ARSENAL YAIPA KIPIGO ‘CHA PAKA JIZI’ LIVERPOOL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top