• HABARI MPYA

    Saturday, April 04, 2015

    YANGA SC WAITOA PLATINUM, WATINGA 16 BORA KOMBE LA SHIRIKISHO

    Na Prince Akbar, ZVISHAVANE
    YANGA SC imetinga hatua ya 16 Bora michuano ya Kombe ka Shirikisho Afrika licha ya kufungwa bao 1-0 na wenyeji FC, FC Platinum Uwanja wa Uwanja wa Mandava, Zvishavane nchini Zimbabwe.
    Kwa matokeo hayo, Yanga SC inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa mabao 5-2 baada ya awali kushinda mabao 5-1 mjini Dar es Salaam.
    Kipa Ally Mustafa Mtinge ‘Barthez’ ndiye aliyekuwa nyota wa mchezo wa leo, baada ya kuokoa hatari nyingi langoni mwake.
    Dakika ya 12, Barthez aliokoa kwa mguu shuti la ‘hapa na hapa’ la Donald Ngoma na mpira ukamkuta Thabit Kamusoko aliyeunganishia nje.
    Kikosi cha Yanga SC kilichoanza leo Uwanja wa Mandava na kufungwa 1-0 na wenyeji FC Platinum, hivyo kufuzu hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikkisho Afrika kwa ushindi wa jumla wa 5-2, baada ya awali kushinda 5-1 nyumbani

    Yanga SC wakajibu kwa shambulizi kali dakika ya 22, baada ya kona ya Simon Msuva kuzua kizaa zaa langoni mwa Platinum. Mpira ulimkuta Amisi Tambwe aliyeunganisha kwa kichwa ukaenda kwa Mrisho Ngassa aliyebinuka ‘tik tak’ ndani ya sita, lakini kipa akapangua kabla ya kuuchupia tena kuudaka.
    Platinum wakafanya shambulizi la kushitukiza dakika ya 28, lakini shuti la Donald Ngoma likatoka nje. 
    Walter Musona aliifungia Platinum bao dakika ya 29 akimalizia pasi ya Ngoma aliyempiga chenga beki Juma Abdul upande wa kulia wa Uwanja.
    Barthez tena akaokoa ndani ya boksi akiwa ana kwa ana Ngoma dakika ya 32. Dakika ya 35 Barthez alidaka shuti kali la Ngoma
    Wachezaji wa Yanga SC wakiwapungia mashabiki wao waliosafiri kwenda kuisapoti timu Zimbabwe

    Yanga SC walijibu dakika ya 53 kwa shambulizi la kushitukiza, Salum Telela akimpelekea pasi nzuri Mrisho Ngassa, aliyewatoka mabeki wawili wa Platinum, lakini akashindwa kupiga kutokana na kubanwa mpira ukatoka nje.
    Safu ya ulinzi ya Yanga ilipata ahueni baada ya Ngoma kutolewa dakika ya 77 nafasi yake ikichukuliwa na Chirwa.
    Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Mbuyu Twite, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Mbuyu Twite, Said Juma/Kevin Yondan dk46, Simon Msuva/Danny Mrwanda dk88, Haruna Niyonzima, Amisi Tambwe, Mrisho Ngassa na Salum Telela. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA SC WAITOA PLATINUM, WATINGA 16 BORA KOMBE LA SHIRIKISHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top